title : ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19
kiungo : ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19
ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumanne tarehe 08-01-2019 .
Akizungumza na waandishi wa habari huko kwenye ukumbi wa Maisara Khuzaimt Bakar Kheir kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Niashati (ZURA) wakati akitoa tarifa kwa umma juu ya mabadiliko ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia kesho tarehe 8-1-2019.
Amesema sababu za mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Desemba ni kwamba bei za mafuta katika soko la Dunia zimeshuka . Mafuta ya Petroli yaliyosafishwa katika soko la Dunia kwa mwezi wa Novemba , 2018 yameshuka kwa Dola za Marekani 137.07 ikilinganishwa na mwezi wa O ktoba 2018.
Pia alieleza kwamba Mafuta Dizeli yaliyosafishwa katika Soko la Dunia ka mwezi wa Novemba 2018 yameshuka kwa Dola za Marekani 115.31 ikilinganishwa na mwezi wa Oktoba , 2018 ambapo mafuta ya Taa (Jet A-1/Keresone ) yaliyosafishwa katika soko la Dunia kwa mwezi wa Novemba 2018 yameshuka kwa Dola za Marekani 96.14 ikilinganishwa na mwezi wa Oktoba 2018.
Aidha alisema aina ya mafuta ya Petroli Bei ya mwezi wa Desemba , 2018 TSHS 2,459 kwa lita ambapo bei ya mwezi wa January 2019 TSHS 2,320 kwa lita tofauti TSH 138.87 sawa na asilimia 5.65%.
Kwa upande wa Dizeli bei ya mwezi wa Desemba , 2018 TSHS 2,539 kwa lita ambapo bei ya January, 2019 2,333 kwa lita tofauti TSH 206.31 sawa na asilimia 8.13%.
Alisema kwenye mafuta ya Taa bei ya mwezi wa Desemba , 2018 TSHS 1,947 kwa lita ambapo bei ya January 2019 TSH 1,787 kwa lita tofauti SHS 160.15 sawa na asilimia 8.23%.
Vile vile kwa upande wa mafuta ya Meli (BANKA) bei ya mwezi wa Desemba , 2018 TSHS 2.367 kwa lita ambapo bei ya mwezi wa January , 2019 TSHS 2,160 kwa lita tofauti TSH 206.31 sawa na asilimia 8.72%.
Hivyo makala ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19
yaani makala yote ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/zura-yatangaza-bei-mpya-za-mafuta.html
0 Response to "ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19"
Post a Comment