WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA .

WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA . - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA ., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA .
kiungo : WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA .

soma pia


WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA .

Abdullatif Yunus - Kagera

Shirika la World Vision Tanzania limekabidhi majengo yaliyojengwa na mradi wa World Vision(Izigo AP) kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji Kabuleme, Kata Izigo, Wilaya ya Muleba.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shule ya Msingi Kabuleme, Meneja Kanda ya Kagera Bi. Juliana Charles ameeleza kuwa mnamo mwaka 2017 mradi wa maendeleo Izigo ulipokea barua kutoka shule ya msingi Kabuleme iliyoainisha matatizo makubwa yanayoikumba shule hiyo, likiwemo tatizo kubwa la uhaba wa madarasa, choo cha wanafunzi na walimu pamoja na madawati. 

Baada ya mradi kupokea taarifa hiyo walifika shuleni hapo na kuona hali halisi ya mazingira ya shule na ufundishaji kwa ujumla. Ndipo walipoandikia andiko na kupitia wafadhiliwa wa nchi ya Ujerumani, andiko liliweza kupata Tzs. 76,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, matundu 5 ya vyoo vya wanafunzi, tanki la maji ya kunawa mikono lenye ujazo wa lita elfu tano, madawati 60 na mipira 6 ya michezo.

Akipokea majengo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Ndg. Emmanuel Sherembi ameendelea kushukuru sana shirika la World Vision Tanzania kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa wilayani Muleba ikiwemo ujenzi na ukarabati wa zahanati ya Bushekya, ujenzi wa zahanati Bugasha, ujenzi wa miundombinu shule ya msingi Kabuleme na ujenzi wa jengo la mama na mtoto kituo cha afya Izigo.

"Msichoke kutufadhili katika sekta za Elimu na Afya kwani Wilaya ya Muleba ina uhaba mkubwa sana wa miundombinu ya Elimu na Afya hali inayopelekea jamii kukosa huduma hizo za muhimu. Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha miundombinu hiyo lakini bado uhitaji ni mkubwa", ameeleza Ndg. Emmanuel Sherembi.

Majengo yaliyokabidhiwa ni pamoja na vyumba vitatu vya madarasa vyenye thamani ya Tzs. 60,132,210.00 ambapo Shirika la World Vision limechangia Tzs. 54,512,210.00 na jamii imechangia Tzs. 5,620,000.00, ujenzi wa matundu matano ya vyoo na ununuzi wa tanki la maji wenye thamani ya Tzs. 14,693,360.00, ununuzi wa madawati 60 kwa jumla ya Tzs. 5,160,000.00 na ununuzi wa mipira 6 ya michezo yenye thamani ya Tzs. 435,000.00. Jumla ya gharama za ujenzi na vifaa ni Tzs.80,420,560.00.
Jengo la Vyumba vitatu vya madarasa vilivyotokana na Mradi wa World Vision - Kagera kwa kushirikiana na Wananchi wa Izigo Muleba.
Picha ya Pamoja, Viongozi wa Halmashauri ya Muleba, World Vision, Kamati ya Shule, walimu na wanafunzi baada ya kukabidhiwa Mradi.
Pichani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Emmanuel Sherembi akizungumza na Wananchi na wanafunzi (hawapo pichani), baada ya kuzindua majengo hayo yaliyojengwa kwa Hisani ya shirika la World Vision.


Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Kagera, Bi Juliana Charles akisoma Taarifa ya Mradi kabla ya Kuukabidhi rasmi.
Pichani ni Meneja Bi Juliana Charles na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Emmanuel Sherembi kwa pamoja wakishirikiana kukata utepe wa jengo la madarasa matatu kama ishara ya Uzinduzi.
Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa World Vision Kagera kwa Shule ya Msingi Kabuleme iliyopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
Picha ya Tanki la Maji lililokabidhiwa.
Jengo la Vyoo vya Matundu matano vilivyokajengwa na World Vision Kanda ya Kagera kwa kushirikiana na Wananchi.


Hivyo makala WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA .

yaani makala yote WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/world-vision-kagera-wakabidhi-madarasa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WORLD VISION KAGERA WAKABIDHI MADARASA, MADAWATI, VYOO NA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI KABULEME - MULEBA ."

Post a Comment