title : WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE
kiungo : WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE
NA LUSUNGU HELELA- KIBAHA
Wizara ya Maliasili na Utalii, imeanza kuyatambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa Fukwe katika Kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Hoteli za kitalii ili kuwavutia watalii kutembelea katika kisiwa hicho.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara hiyo kuwa ianzishe Kurugenzi ya Fukwe itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza Fukwe zote nchini.
Lengo likiwa ni kuhakikisha mapato yatokanayo na sekta ya Utalii kupitia Utalii wa Fukwe yanaongezeka kwa mfano Kisiwa cha Mafia ni cha tano duniani kwa uzuri wa vivutio vya utalii na rasilimali bahari na cha pili barani Afrika, Hivyo kina sifa kemkem za kuongeza pato la Taifa zaidi.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya siku mbili kisiwani humo ya kutembelea Fukwe pamoja na magofu ya kale, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema Wizara imejipanga kikamilifu kwa ajili kuwasaidia Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye Fukwe kwa ajili ya utalii.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Kanyasu alitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo kisiwani humo ukiwemo Msitu wa Mlola, Magofu na fukwe katika kijiji cha Kanga pamoja na maeneo ya uwekezaji ya Ras Mlundo Jojo, Banja, Rasini Kanga na Tembo Unyama.
Hata hivyo, Baada ya ziara hiyo Naibu Waziri huyo alisema kuwa baadhi ya wamiliki wa maeneo hayo ya fukwe yamefanya kuwa mashamba ilhali ni kivutio kikubwa cha utalii ambapo baadhi ya nchi zimekuwa ziikingiza fedha nyingi za kigeni kupitia utalii wa fukwe.
Aidha, Kanyasu amewataka wananchi wanaomiliki maeneo karibu na Fukwe kuyatumia kwa ajili ya utalii wa fukwe badala ya kuyageuza kuwa mashamba.
Amesema kuwa watalii walio wengi kutoka nje za nchi mara baada ya kutembelea Hifadhi za Taifa kama vile Serengeti Mikumi, husafiri kwenda Msumbiji au Zanziba' kwa ajili ya kutembelea Fukwe ilhali kuna fukwe nzuri mbali na Kisiwa cha Mafia ambazo hazijaweza kuendelezwa
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaib Nnunduma alieleza kuwa wilaya yake inawakaribisha Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika wilaya hiyo na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha.
Aliongeza kuwa Wilaya hiyo tayari imeshatenga maeneo kwa ajili ya Wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za kiutalii katika maeneo ya ufukweni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ( watatu kulia) akiwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama akipewa maelezo na Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi, Maliasili na Utalii, Juma Hassan kuhusu eneo la fukwe lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa ujenzi wa Hoteli za kitaliii wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa Fukwe katika wilaya ya Mafia mkoani Kibaha.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mohammed Kongo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea maeneo ya fukwe ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa
ianzishe Kurugenzi ya Fukwe
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akishuka kwenye ndege ndogo wakati alipowasili wilayani Mafia mkoani Kibaha kwa ajili ya kutembelea maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji wa Utalii
Baadhi ya rasilimali bahari maarufu kwa jina la Matumbawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ( kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Mafia pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya fukwe yanayofaa kwa ajili ya uwekezaji lengo likiwa ni kuhasisha utalii wa fukwe
Moja ya magogfu ya kale lililojengwa karne ya 18 ambalo linapatikana pembezoni mwa fukwe katika kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mafia. Erick Mapunda akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu kabla hya kufanya ziara ya kutembelea maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji wa utalii.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
Hivyo makala WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE
yaani makala yote WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wizara-ya-maliasili-na-utalii-yaanza.html
0 Response to "WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE"
Post a Comment