title : Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma
kiungo : Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma
Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma
Jumla ya nyumba Mia Moja za Makazi ya Askari zimeanza kujengwa mkoani Dodoma ikiwa ni Mpango wa serikali kukabiliana na changamoto za makazi ya Askari Polisi watakaohamia hivi karibuni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza agizo la kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani hapa
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama kutembelea eneo la Medeli Mashariki ambapo Awamu ya Kwanza ya mradi huo ukihusisha nyumba 30, Ujenzi wa Shule ya Awali, Ujenzi wa Kantini, Ujenzi wa Viwanja vya Michezo tayari imeshaanza
“Ujenzi wa nyumba hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa nyumba kama hizi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha askari wanaishi sehemu safi na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ujenzi wa nyumba kama hizi kote nchini unafanyika kwa gharama nyepesi na tukitumia wataalamu wa ujenzi waliopo serikalini na katika Jeshi la Polisi..” alisema Masauni
“…..mradi huu utakua na awamu tatu ambapo mwezi April mwaka jana, awamu ya kwanza ilianza na kutarajiwa kukamilika April mwaka huu huku awamu zilizobakia zikitarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu na hadi kufikia mwaka kesho katikati awamu zote zitakua zimekamilika” aliongeza Masauni
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu amewapongeza Viongozi wa wizara na Jeshi la Polisi kwa mradi huo huku akishauri miradi mingine wajenge maghorofa ili kuweza kuitumia ardhi waipatayo kwa matumizi mengine sambamba na ujenzi wa makazi ya askari.
“Nawapongeza kwa kutumia mapato yenu wenyewe ya ndani kuanzisha miradi mikubwa kama hii na sisi wajumbe wa kamati tumeridhishwa na hatua hizi za kukabiliana na makazi ya wapiganaji wetu wanaotulinda usiku na mchana na nchi yetu kuendelea kuwa na amani,” alisema Zungu
Jumla ya gharama ya mradi huo wa nyumba Mia Moja za Makazi ya Askari Polisi ni Bilioni Mia Tatu na Laki Tano ambazo zinatokana na Mfuko wa Tuzo na Tozo ikiwemo malipo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na askari polisi na faini zinazotozwa na askari kwenye makosa mbalimbali.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akitoa maelezo ya Ujenzi wa Nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu akimuuliza maswali Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli,jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja(pichani) kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Ihumwa ,jijini Dodoma yanapojengwa Makao Makuu ya wizara hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika eneo la Medeli ikiwa ni mkakati maalumu wa Serikali ya Awamu ya Tano kujenga makazi ya askari polisi nchi nzima ili kuwaondolea askari changamoto za makazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Hivyo makala Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma
yaani makala yote Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/bilioni-35-kujenga-makazi-ya-askari.html
0 Response to "Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma"
Post a Comment