title :
kiungo :
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga Ummy Mwalimu leo ameweka jiwe la Msingi kwenye madarasa sita shule ya Msingi Mwakidila Jijini Tanga yaliyofadhiliwa na Ubalozi wa Japani nchini.
Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Waziri Ummy kuhakikisha anashirikiana na wananchi wa Jiji la Tanga kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa kwa shule zenye uhaba ili kuwawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo.
Mradi wa ujenzi huo uliofadhiliwa na Ubalozi wa Japani nchini Tanzania kupitia shirika la TAWODE (Tanga Women Development Initiative) una thamani ya shilingi Milioni 179,777,898.00 pamoja na madawati 180 mpaka kumalika kwake.
Akizungumza katika halfa hiyo Waziri Ummy alisema baada ya kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo darasa moja kwenye shule hiyo lilikuwa likikaa wanafunzi 166 ndipo alipoamua kuweza kuishughulikia changamoto hiyo kwa vitendo na kufanikiwa kupata ufadhili huo ambao umewezesha ujenzi huo.
Halfa hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniue,madiwani na viongozi mbalimbali wakiwemo wa idara ya Elimu Jiji hilo wakiwemo viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga wananchi,walimu na wanafunzi.
Alisema kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli inastahili kupongeza kila wakati kutokana na kuanzisha sera ya elimu bure ambayo matokeo yake yameanza kuonekana kutokana na kuwepo kwa ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza Jijini Tanga mwaka huu.
“Kwa mujibu wa takwimu za Jiji la Tanga uandikishaji wa wanafunzi wa shule ya Msingi umeongezeka kutoka mwaka 2015 watoto 8495 hadi watoto 10345 mwaka 2018 na ongezeko hilo sio kwa sababu watu wanazaa sana kutokana na kwa mujibu wa takwimu zao kiwango cha wanawake kuzaa watoto kimepungua sana kuliko zamani mwanamke anaweza kuzaa watoto mpaka saba.
Alisema kwamba kwa sasa mwananke mmoja anaweza kuzaa watoto kati ya watano na hao walikuwa majumbani na walikuwa hawaendi shule kutokana na kukwamishwa na ada na michango mbalimbali ambayo awamu hii imeamua kuiondoa na hivyo wananchi kuweza kuwapeleka watoto wao shuleni kutokana na sera ya elimu bure bila malipo.
Aidha aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli ili aweze kuendelea kuijenga Tanzania mpya ya viwanda kwa vitendo kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo
“Ndugu zangu wana Tanga Rais wetu Mh Dkt John Mgufuli amefanya kazi kubwa sana kuhakikisha watoto wanapata elimu na kila mwezi amekuwa akitoa milioni 54 kwa shule za msingi Jiji la Tanga na Milioni 55 kwa shule za Sekondari kwa ajili ya kuhakikisha watoto wanasoma bila malipo hivyo niwaambieni tutamlipa kwa kazi kubwa na mazuri kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya
tumuonyeshe kwa vitendo kwenye serikali za mitaa kwamba tupo pamoja naye”Alisema Waziri Ummy.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Waziri Ummy ambako kwa Jiji hilo wanajivunia sana kuwa na kiongozi kama yeye kutokana na namna alivyojitoa kusaidia maendeleo huku akimuhaidi kuchangia tiles kwa madarasa hayo sita.
Alisema kwa kipindi cha mwaka 2018 waliandikisha wanafunzi darasa la kwanza asilimia 121 ya lengo ambalo walikadiria kuandikisha akwani walikaadiria wanafunzi 8506 na waliweza kuandikisha10345 hali inayonyesha mwitiko mkubwa wananchi kuwapeleka waoto shule.
Alisema hali hiyo miaka ya nyuma hakuwepo huku akieleza mwitikio huo wananchi watahakikisha wanaweka miundombinu sambamba na watoto wanaondikishwa kwenye shule hizo ili waweze kupata sehemu ya kusomea.
Hata hivyo alitoa wito kwa wazazi na wananchi kushirikiana na serikali kujenga miundombinu ya shule ili kuweza kuhakikisha wanafunzi wanaondikishwa kujiunga na darasa la kwanza wanapata fursa ya kusoma
“Lakini pia nimshukuru Rais kwa kuleta mpango wa elimu bila malipo kwani kwa kipindi cha miaka miwili shule za msingi zimepokea milioni 984.8 kama ruzuku inayokwenda moja kwa moja kwa shule kutekeleza mpango elimu bila malipo…2017/2018 milioni 656.8 ziliwekwenda moja kwa moja shule za msingi na mwaka 2018/2019 wamepokea kuanzia desemba milioni 325 mpango huu umeweza kuwasaidia shule zao kwenye mambo mengi “Alisema.
Pia alisifu jitihada kubwa zinazofanywa na Waziri Ummy kuhakikisha anakuwa mstariu wa mbele kutatua changamoto za wananchi licha na kuwa na majukumu makubwa lakini umekuwa akitujali watu wa Tang.
Mkurugenzi huyo alisema katika Jij la Tanga kuna shule za msingi 104 za serikali 79 changamoto nyingi za hali ya miundombinu shule za msingi za Jiji la Tanga mahitaji ya vyumba vya madarasa 1251 lakini vilivyopo 710 upungufu ni vyumba 541.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/waziri-wa-afya-maendeleo-ya-jamii.html
0 Response to " "
Post a Comment