WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI
kiungo : WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI

soma pia


WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mke wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Bin Zubeir yaliyofanyika Kwamndolwa, Korogwe mkoani Tanga.

Akitoa salam kwa niaba yake amesema “Rais Dkt. Magufuli aliweka nia ya dhati kushiriki mazishi haya ila kwa bahati mbaya leo ana mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha ambapo yeye ni Mwenyekiti.” 

“Mheshimiwa Rais amenituma nije nikupe pole wewe, watoto, familia na wote walioguswa na msiba huu. Mheshimiwa Rais anawaombea kwa Mungu ili mpate utulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na nguzo katika familia. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”

Waziri Mkuu ameshiriki mazishi hayo ya mke wa Mufti, Bibi Hidaya Omar leo (Alhamisi, Januari 31, 2019).

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasihi wafiwa na waombolezaji wote waendelee kuwa watulivu na kumuombea marehemu kila mmoja kwa imani yake ili Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumtuma Waziri Mkuu amuwakilishe katika mazishi hayo. Pia amewashukuru watu wote waliojitokeza kwa ajili ya kuifariji familia kutokana na msiba walioupata.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo niWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, Mhe. Salma Kikwete, Mhe. Hawa Ghasia, Mhe. Mary Chatanda ,Mhe. Mkuu wa Mkoa wa TangaMartine Shigelana Masheikh wa Mikoa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika mazishi ya Hidaya Omar, mke wa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubier  yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki katika sala ya jeneza  wakati wa mazishi ya Hidaya Omar, Mke wa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeir  (kushoto kwa Waziri Mkuu) yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Sheikh Mohammed Kigoda aliyeongoza sala hiyo na kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Alhad Mussa Salum. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeir  baada ya kushiriki katika mazishi ya Hidaya Omar, mke wa Mufti ,yaliyofanyika  katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.


Hivyo makala WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI

yaani makala yote WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/waziri-mkuu-amuwakilisha-rais-mazishi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI"

Post a Comment