TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA
kiungo : TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

soma pia


TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.

Brig. Jen. (rtd) Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu ya Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

“TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.

Ameongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali mkoani hapa.

Kafulila amesema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Mhandisi Cosmas amesema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana katika Mikataba.
 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila akisaini mikataba ya Ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, ambapo Wakala wa Majengo (TBA) wamekubali kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano na kwa gharama ya shilingi bilioni moja.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.


Hivyo makala TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

yaani makala yote TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/tba-kamilisheni-miradi-kwa-wakati-rc.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA"

Post a Comment