WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA

WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA
kiungo : WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA

soma pia


WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na soko la mazao la OTC-Lilambo katika Halmashauri ya Songea uliogharimu sh. bilioni 1.5.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala pa uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili kuwaongezea tija.Amefungua soko hilo leo (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala kwani umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka.“Licha ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia mazao yao, pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja na taarifa za masoko.”Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao yao sokoni hapo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua  Soko la Mazao   la OTC Lilambo  wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Watatu kushoto ni Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani Msongozi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua  Soko la Mazao   la OTC Lilambo  wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro,  wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilitokana na unga wa mhogo vilivyoandaliwa na kikundi cha wanamawake wajasiriamali cha  Muungano - Mpandagindo,   wakati lipofungua  Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za nafaka  la OTC Lilambo wilayani Songea ambalo lilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali  vilivyoandaliwa na kufungashwa kitaalam  na Mtandao wa Wajsiriamali Wadogowadogo Ruvuma (MWARU) wakati alipofungua  Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani  Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Mtandao wa MWARU, Lucida Chowo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .




Hivyo makala WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA

yaani makala yote WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/waziri-mkuu-afungua-soko-la-mazao-songea.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA"

Post a Comment