title : WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI.
kiungo : WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI.
WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga(aliyesimama)akitia nasaha za ufunguzi wa Kikao kazi cha watumishi wa taasisi hiyo jijini DSM.
Mkurugenzi wa Programu za TASAF,Bw. Amadeus Kamagenge (aliyeshika kipaza sauti) akitoa mada kwenye kikao kazi cha Watumishi wa Taasisi hiyo juu kukamilika kwa awamu ya kwanza na maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini-PSSN.
Mmoja wa Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF akisoma taarifa ya pamoja ya utekelezaji wa maafisa hao kwenye kikao kazi kilichoanza hapo jana jijini DSM.
Baadhi ya Watumishi wa TASAF akiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa taasisi hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani kwenye kikao kazi ambacho hufanyika kila mwaka kujadili utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa taasisi hiyo wanaohudhuria kikao kazi kinachojadili utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo jijini DSM.
Na Estom Sanga- DSM.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wamekiri kuwa usimamizi na miongozo thabiti inayotolewa na Serikali imechangia kwa kiwango kikubwa kufanikiwa kutekelezwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na Umaskini.
Akifungua kikao kazi cha Wafanyakazi wa Mfuko huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo yamechangia jitihada za Serikali za kukuza na kuboresha maisha ya wananchi hususani wale ambao wamekuwa wakiishi katika dimbwi la umaskini na kuamsha ari ya wao kujiletea maendeleo.
Bwana Mwamanga amewaasa Watumishi hao wa TASAF kutobweteka na mafanikio yaliyopatikana katika kuwahudumia Walengwa wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini badala yake waongeze jitihada zaidi ili lengo la Serikali la kupambana na adui umaskini liwe la mafanikio endelevu na makubwa zaidi kupitia Mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amebainisha kuwa maelekezo ya Serikali katika kusimamia na kuboresha utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa awamu ya pili yakiwemo ya kuwashirikisha Walengwa Kufanya kazi yatazingatiwa ili kukuza kipato cha Walengwa hao na kuwawezesha kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa taifa na kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo yao.
Bwana Mwamanga amesema kuwa kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika awamu yake ya kwanza , kumekuwa na mahitaji kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao Mpango huo haujawafikia wakitaka wajumuishwe kwenye huduma za Mpango huo ambapo amesisitiza kuwa maelekezo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Wananchi wenye uhitaji na kuwa na vigezo vya kujumuishwa kwenye Mpango wapate huduma hiyo kazi ambayo amesema itatekelezwa katika awamu ijayo ya Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini.
Katika awamu ya kwanza ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa na kuendelea kupata huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF -ambayo ni sawa na asilimia 70 ya vijiji/shehia huku asilimia 30 ya vijiji/shehia ikisalia kutokana na ufinyu wa raslimali fedha.
Akitoa taarifa ya kukamilika kwa Awamu ya Kwanza ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na Maandalizi ya Sehemu ya Pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, Mkurugenzi wa Programu za Jamii wa TASAF, Bwana Amadeus Kamagenge ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu ya kwanza kuwa ni pamoja na kuanzisha Masjala ya Walengwa zaidi ya Milioni Sita huku kazi ya kuhaulisha fedha ikitekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa Walengwa tangu mwaka 2014.
Aidha amesema Serikali kupitia TASAF imefanikiwa kuhamasisha Wananchi ambao walikuwa wakiishi katika umaskini mkubwa kurejesha matumaini kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali kwa kutumia sehemu ya ruzuku huku wakitekeleza masharti ya Mpango hususani yanayolenga katika sekta za Elimu na Afya na hivyo kujiongezea uwezo wa kukabiliana na kero ya umaskini.

Hivyo makala WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI.
yaani makala yote WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/watumishi-tasaf-waoanisha-mafanikio-ya.html
0 Response to "WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI."
Post a Comment