WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB

WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB
kiungo : WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB

soma pia


WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB

SHINDANO la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata', leo limeendelea kuchezeshwa huku wateja sita wakijishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja.

Katika droo hiyo ya nne pia wateja 20 wengine wa benki hiyo wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- ambazo zitaingizwa kwenye akaunti zao moja kwa moja ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo. Droo hiyo ya nne iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imefikisha wateja 80 hadi sasa ambao wameshindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchezeshwa droo ya leo, Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala alisema mbali na droo hiyo kupata washindi 20 wa shilingi 100,000/- kila mmoja, wateja 6 wengine wamejishindia simu aina ya Samsung S9+' kila mmoja yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/-.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.

Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano hilo.

Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika kwenye tawi lake.

Meneja kutoka kitengo cha Kadi cha Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa (kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya nne ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo na Domitila Silayo wa NMB (kushoto).

Mtaalam kutoka kitengo cha Kadi cha NMB, Domitila Silayo (kulia) akiwasiliana na mmoja wa wateja wa NMB waliojishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kwenye droo ya nne ya Shindano la MastaBata. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo pamoja na Sophia Mwamwitwa wa NMB akishuhudia (kushoto).
Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kufafanua wateja walivyojishindia zawadi anuai kwenye Masta Bata ya NMB.


Hivyo makala WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB

yaani makala yote WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wateja-6-wajishindia-simu-samsung-s9.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATEJA 6 WAJISHINDIA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB"

Post a Comment