SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES
kiungo : SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

soma pia


SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

Na Munir Shemweta, KOROGWE 

Serikali imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12,915.126 ya kampuni ya Mohamed Enterprises yaliyopo korogwe mkoa wa Tanga. 

Uamuzi wa kufuta mashamba hayo unafuatia mapendekezo yaliyotolewa na halmashuri ya wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu na baadaye maombi hayo kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wizara kwa nia ya kufutwa. 

Mashamba yaliyofutwa ni yale yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge wilayani Korogwe mkoani Tanga. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba hayo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula alisema mashamba yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohamed Enterprises Mazinde wilayani Korogwe na kubainisha kuwa uamuzi huo unalenga kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali kuzingatia masharti ya uwekezaji. 

Alisema, mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba ya Mohamed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji juu ya mambo ya halmashauri husika la kutoendelezwa mashamba na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo kwa rais na kuridhiwa. 

Alisema, uamuzi huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohamed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji. 

Hata hivyo, Dk Mabula alisema mashamba ambayo hayajabatilishwa yamewekewa utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa nia ya kufanya vizuri. 

Ameitaka halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la serikali ni kuwa na uwekezaji wa viwanda.

Aidha, Dk Mabula alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kwa kufanya kazi nzuri ya kufutilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais John Pombe Magufuli alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga. 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela aliwataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo. 

Alisema, ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi na uwekezaji. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
Mkazi wa Mabogo Korogwe mkoani Tanga Said Mbazi Idawa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula katika Mashamba ya Mkonge Korogwe mkoa wa Tanga.
aibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa Tanga wakati alipotembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019.
Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed Enterprises lilipo Korogwe mkoani Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika shamba lilipo eneo la Mabogo Korogwe Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa wakimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kuangalia eneo la mashine za kutengeneza katani katika shamba la Mohamed Enterprises lililopo Mabogo Korogwe mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)


Hivyo makala SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

yaani makala yote SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/serikali-yafuta-mashamba-sita-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES"

Post a Comment