title : WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA
kiungo : WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA
WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA
Na. Vero Ignatus, Arusha.
Wito umetolewa kwa wasanii nchini kujisajili katika Baraza na sanaa nchini ili waweze kutambulika, kupata haki zao msingi, na wawe na uhuru wa kufanya kazi
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Katibu wa Shughuli za Sanaa Kanda ya Kaskazini Flora Mgonja ambapo amewataka wasanii kufahamu kuwa sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na wanatakiwa kuithamini, kuipenda na kuilinda
Amesema sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyoanzishwa kwa mujibu wa Bunge na kanuni mpya ya Februari 2018 inamtambua msanii, inaelezea sababu ya msanii kusajiliwa, pia zimeweka wazi kwamba hakuna msanii yeyote ambae anaweza kufanya kazi zake bila kusajiliwa Basata
Kwa mujibu wa Kanuni za Baraza la sanaa la Taifa, 23-(1)Mtu yeyote hatoruhusiwa kufanya kazi ya sanaa ya aina yeyote kwa mujibu wa sheria inayohusika na sanaa, kufanya biashara ya kazi za sanaa bila kusajiliwa na Baraza
Amesema kuwa Baraza la sanaa la Taifa lipo tayari kuwasaidia pele watakapokuwa wamesajiliwa na kutambuliwa ili kuweza kuwapa huduma kwa mujibu wa sheria na taratibu.'' Tuna dawati la sheria pale ofisini kwetu hawalijui wasanij wengi, wanadhukumiwa mikataba, wanashindwa kupata fidia zao kwasababu hawajasajiliwa, leo unakuja kusema kazi yangu imechukuliwa wakati hujasajiliwa''
Amesema kwa sasa wameanza kutoa elimu kwanza kwa wasanii mbalimbali katika kanda zote sita nchini ambapo kila mmoja wapo anatakiwa kutambua kwamba anatakiwa ajisajili kwenye Baraza la sanaa la Taifa.' 'Hatuwezi kuwabana tukakimbikia kwenye sheria, tunamuda ambao tumejiwekea kuhakikisha kwamba msanii ajitambue kwamba ni lazima nisa jiliwe kwenye Baraza la sanaa la Taifa"Alisema
Amesema wanapoelekea itafikia mahala ambapo washehereshaji (MC) wote,Dj, kufanya kazi bila kuwa na cheti kutoka Basata kwani wasanii wote wanatakiwa wawepo kwenye Data base.Amewataka kufahamu kuwa kujisajili kwao ni fursa, kwani baraza hilo linanafasi ya kumsaidia msanii pale anapopata mialiko mbalimbali ya kwenda nje ya nchi kufanya matamasha nchi za nje
Amesema kwa sasa msanii hawezi kupita uwanja wa ndege bila barua kutoka Basata kama anakwenda nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni na sheria za Baraza la sanaa la Taifa
'' Lazima msanii apate barua na ada yake ni shilingi 50,000Msanii anapoondoka nchini kwenda nje ya nchi anatakiwa aondoke na kibali kutoka basata ambacho ni shilingi 50,000 akiwa na tatizo lolote nchi husika zinawasikiana lakini akiondoka. Kiholela hawezi kusaidika''alisisitiza
Ameainisha garama za kujisajili kwa msanii ni shilingi 45,000, mchanganuo wake fomu 5000, usajili 20,000, kibali cha mwaka 20,000 ambapo jumla yake ni 45,000 .Sambamba na hayo amesisitiza kuwa usajili kwa msanii binafsi ni mara moja kwa mwaka, ila kibali cha mwaka kinalipiwa kila mwaka mpya unapoaanza.
Mratibu wa shughuli za sanaa Kanda ya Kaskazini Flora Mgonja akiwa katika ofisi ya Utamaduni Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
Kutoka kulia ni Mratibu wa shughuli za Sanaa Kanda ya Kaskazini (BAATA) Flora Mgonja, akiwa na Msimamizi wa maendeleo ya sanaa Kanda ya Kaskazini - BASATA. Picha na Vero Ignatus
Kutoka kulia ni Afisa michezo na Utamaduni Jiji la Arusha Benson B. Maneno, Mratibu wa shughuli za sanaa Kanda ya Kaskazini (BASATA) Flora Mgonja na Msimamizi wa maendeleo ya sanaa Kanda ya Kaskazini -BASATA
Hivyo makala WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA
yaani makala yote WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wasanii-jisajilini-mpate-haki-zenu-za.html
0 Response to "WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA"
Post a Comment