WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA

WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA
kiungo : WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA

soma pia


WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA



Na Rhoda Ezekiel,Kigoma

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Kichacha katika Kijiji cha Kichacha Kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameipongeza Serikali kwa kuwajengea madarasa na kuwatoa chini ya mti walikokuwa wakisomea awali.

Pongezi hizo wamezitoa jana baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala kutembelea shule hiyo na kukuta watoto wakiwa katika vyumba vya madarasa tofauti na awali walipokuwa wakisomea katika nyumba ya miti.

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo Kulwa Anania amesema walikuwa wakipata wakati mgumu pindi mvua zilipokuwa zikinyesha kwani walikuwa hawaendi shule kwa kuwa walikuwa hawana eneo zuri la kusomea na ilikuwa ikisababisha kushuka kwa ufaulu katika masomo.

Amesema wanaipongeza Serikali kwa kutatua changamoto yao waliokuwa nayo na sasa wanaendelea kusoma vizuri katika mazingira mazuri na wanaipongeza serikali kwa jitihada wanazo zifanya.Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kichacha Emanuel Siwija amesema kwa mwaka 2017/2018 walipokea jumla ya Sh. milioni 42 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na vyoo matundu manne na ofisi moja, ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika na wanafunzi wanatumia vyumba hivyo.

Amesema awali wanafunzi hao walianza kusomea chini ya mti ,na baadae wakajenga kijumba cha miti kwa ajili ya kujihifadhi na 2018 ndipo walipopata madarasa na mpaka sasa upungufu ni mdogo.Ameongeza kwa mwaka jana wao kama shule kwa matokeo ya darasa la nne wameshika nafasi ya pili katika Wilaya na wanaendelea kupambana kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa kuwa nyenzo za kufundishia wanazo na Serikali imetoa madawati kupitia Mkuu wa Wilaya.

Akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, amesema wao kama Serikali wamejitahidi sana kuhakikisha suala la upungufu wa vyumba vya darasa linapungua na kuhakikisha Wanafunzi wanapata elimu na katika mazingira bora ya kusomea .

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kuchangia shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao.

Aidha Mkuu huyo alitoa mwito kwa Wananchi wa Wilaya hiyo kuwapuuza Wale wote wanaowashawishi wananchi kuacha kujitolea katika shughuli za maendeleo kwa kuwa maendeleo yote yanaletwa na Wananchi kwa kushirikiana na Serikali.


Shule ya msingi Kichacha ilivyokuwa mwaka 2017

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kichacha katika Kijiji cha Kichacha Kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Kanali Ndagala ametembeea shule hiyo na kukuta watoto wakiwa katika vyumba vya madarasa tofauti na awali walipokuwa wakisomea katika nyumba ya miti.
Shule ya msingi Kichacha ilivyo sasa 


Hivyo makala WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA

yaani makala yote WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wanafunzi-shule-ya-msingi-kichacha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA"

Post a Comment