title : MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA
kiungo : MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA
MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA
*Asema ndoto yake ni kuona TANESCO inajiendesha kwa faida,kutoa gawio kwa Serikali
*Aelezea mkakati wao ni kuendelea kuboresha huduma ya umeme, agusia miundombinu
*Akerwa na tabia ya kuchoma moto katika maeneo ambayo miundombinu yao inapita
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Dk.Tito Mwinuka amewahimiza watumishi wote wa shirika hilo kutoa huduma bora ,sahihi na kwa wakati kwa wateja wao huku akieleza ndoto yake ni kuona shirika hilo linajiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa Serikali.
Dk.Mwinuka ameeleza hayo mjini Arusha, wakati anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme inayotokelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli .
Ziara hiyo imefanyika katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro na miongoni mwa miradi ambayo wahariri wameona ilivyotekelezwa ni ile iloyopo kwenye TEDAP.
Akifafanua zaidi wakati anajibu baadhi ya maswali ya wahariri hao.Dk.Mwinuka amesema pamoja na kuwepo kwa pongezi nyingi zinatokana na kuwepo kwa huduma bora zinazotolewa na shirika hilo lakini bado amesisitiza kwa watumishi wote wa TANESCO kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja.
"Tunataka kuona TANESCO inatoa huduma nzuri na hiyo iwe kwa nchi nzima.Tunataka mteja anapokwenda TANESCO au kokote ambako tunatoa huduma basi apate huduma nzuri,sahihi na kwa wakati pamoja na kuheshimiwa.Hivyo niendelee kutoa rai kwa watumishi wa ngazi zote tuliyopo tutoe huduma nzuri,"amesisitiza.
Alipoulizwa kuhusu ndoto yake ,Dk.Mwinuka amejibu kuwa ndoto yake ni kuona TANESCO inajiendesha na kufanya kazi zake kwa faida na kwamba wanakwenda vizuri huku akifafanua kwa miaka miwili sasa shirika hilo linajiendesha bila kupewa ruzuki.
" Malengo yetu ni kuhakikishia TANESCO tunafanya kazi zetu na kutengeneza faida na hii imeanza kuleta tija,ni mwaka wa pili tunajiendesha bila ruzuku ya Serikali na hiki ndicho tunachosisitiza tuwe shirika ambalo linapata faida na hatimaye tutoe gawio kwa Serikali," amefafanua Dk.Mwinuka.
Kuhusu madeni ,Dk.Mwinuka ameweka wazi TANESCO ilikuwa inadaiwa madeni makubwa ambayo yaliionekana sugu lakini kupitia mikakati yao wamedhamiria kulipa madeni hayo na kwamba kwa sasa wamefanikiwa kwani deni haliongezeki na hivyo wanatarajia kuyamaliza.
"Kutokana na hali iliyokuwepo miaka ya nyuma TANESCO ilijikuta inadaiwa ,hivyo tunaendelea kulipa madeni ya nyuma," amesema na kusisitiza pamoja na muelekeo mzuri wa shirika hilo bado wamejipanga kutoa huduma ikiwemo ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umeme wa uhakika na kuendelea kutatua changamoto zilizopo.
Kuhusu miradi ya Miradi ya Kuimarisha mifumo ya Usambazaji Umeme nchini(TEDAP) Dk.Mwinuka amesema wamefanikiwa kuitekeleza miradi hiyo kwa mikoa ya Arusha,Kimanjaro na Dar es Salaam na kwamba uwepo wa miradi hiyo imeleta tija kubwa.Alipoulizwa iwapo TANESCO itapeleka mradi wa TEDAP katika mikoa mingine ,Dk.Mwinuka amesema kuwa "Ni kweli tunatamani kuipeleka miradi hiyo nchi nzima maana tumeona faida yake kwa mikoa ambayo tuimeitekeleza.
"Pamoja na kutamani TEDAP itekelezwe na kwenye mikoa mingine lakini changamoto kubwa ni fedha.Hata hivyo pamoja na changamoto hiyo TANESCO tumejiongeza kwani kwa kutumia fedha zetu za ndani tumeutekeleza mradi wa TEDAP eneo la Dege Kigamboni.Hivyo tutaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa umeme," amesema Dk.Mwinuka.
Pamoja na mambo mengine wahariri walitaka kufahamu kuhusu uchomwaji moto maeneo ambayo imepita miundombinu ya TANESCO,amejibu kuwa ni kweli kuna mikoa uchomaji moto umeshika kasi na kuitaja baadhi ya mikoa hiyo ni Lindi,Mtwara na Songea ambako huko ndiko mto unaonekana kuwaka sana.
" Wananchi wasichome moto katika maeneo ambayo miundombinu ya umeme, ni jukumu letu sote kuhakikisha tunailinda na kuitunza miundombinu yetu ya umeme ambayo uwekezaji wake katika kutekeleza miradi ya umeme inatumia gharama kubwa.Tuitunze miundombinu yetu,"amesema Dk.Mwinuka.
Wakati huo huo Dk.Mwinuka amezungumzia namna ambavyo wakati mwingine TANESCO inatupiwa lawama katika jambo ambalo huenda halikusababishwa na Shirika hilo.Ametoa mfano unapotokea moto lawama mara nyingi zinaelekezwa TANESCO hata kama chanzo cha moto ni mteja wao.
"Mtu anaweka pasi kwenye umeme,halafu anapomaliza kunyoosha nguo hazimi swichi ya umeme,ikitokea bahati mbaya kukatokea moto lawama zinakwenda TANESCO wakati sababu za moto ni mteja.Hata hivyo hatuwezi kukwepa moja kwa moja ,hivyo sote tunaotumia umeme kuchukua tahadhari kuondoa hizi lawama," amesema Dk. Mwinuka na kuwaomba wateja wao kuwa sehemu ya kuondoa tatizo la moto.
Kuhusu TANESCO kutumia magrupu ya WhatsApp kutoa taarifa kuhusu umeme kwa wateja wao,amesema magrupu hayo yanasaidia sana kutoa taarifa kwa haraka na uhakika.Ametoa rai kwa TANESCO kwa wilaya na mikoa yote nchini kuhakikisha kunakuwa na magrupu hayo na kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga nayo kwa lengo la kutoa na kupokea taarifa zinazohusu umeme nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto), akiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughhulikia usambazaji na huduma kwa wateja, Mhandisi Raymond Seya, (wakwanza kulia), Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, wakati akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliokuwa wakitembelea mradi wa ukarabati na uimarishaji miundombinu ya umeme, TEDAP, na ule wa Kenya-Tanzania Power Interconnection Project (KTPIP) TII jijini Arusha.
Dkt. Mwinuka na wasaidizi wake, wakiwa na wahariri.
Dkt, Mwinuka akisikilzia kwa makini maoni na maswali kutoka kwa wahariri
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akifungua kikao hicho.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stella Hiza, akijitambulisha. Picha na K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha

Hivyo makala MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA
yaani makala yote MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mkurugenzi-mtendaji-wa-tanesco-abeba.html
0 Response to "MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA"
Post a Comment