title : WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA
kiungo : WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA
WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA
ZAIDI wa Wachama Wastaafu 5000 mkoani Tanga waliondikishwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia Julai 2009 hadi Septemba 2018 wameanza kuhakikiwa.
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Mfuko mkoani Tanga Ally Mwakababu (Pichani Juu) wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema zoezi hilo lilianza Januari 2 mwaka huu na litamalizika Machi 30 mwaka huu.
Alisema kwamba uhakiki huo unafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu huku akiwataka wastaafu mkoani hapa ambao walioandikishwa kufika kwenye ofisi za mfuko huo kwa ajili ya kuhakikiwa.
“Mwanachama Mstaafu afike ofisini akiambatana na mwenza wake (endapo yupo hai)endapo mwanachama mstaafu amefariki ,mwenza aliyebaki afike kwa ajili ya uhakiki huo “Alisema Meneja huyo.
“Lakini pia mwanachama anapaswa kufika na vitu muhimu ikiwemo kitambulisho cha NHIF, Cheti cha Ndoa (kwa mstaafu mwenye mwenza),Kitambulisho cha Uraia au mpiga kura ,leseni ya Gari au hati ya kusafiria ikiwemo barua ya kustaafu “Alisema Meneja huyo.
Hata hivyo alisema kwamba ofisi inawataka wanachama wastaafu kufika kwa uhakiki ndani ya muda uliowekwa ili kuepuka usumbufu wa kukosa huduma kwa kutokufanya hivyo.
Hivyo makala WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA
yaani makala yote WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wanachama-wastaafu-wa-mfuko-wa-taifa-wa.html
0 Response to "WANACHAMA WASTAAFU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA WAHAKIKIWA"
Post a Comment