VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU

VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU
kiungo : VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU

soma pia


VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU


NA DENIS MLOWE, IRINGA

MWENYEKITI wa Serikali za vyuo vikuu vya Kikatoriki chini, Anord Mvamba ametoa wito kwa vijana kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vinavyowalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu sanjari na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo hatua itakayowasaidia kufikia malengo yao.

Ametoa rai hiyo juzi mara baada ya kujumuika pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tosamaganga kilichoko wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Mvamba alisema kuwa kundi la watu wasiojiweza wanahitaji kupata misaada kutoka kwa jamii inayowazunguka na hasa vijana ambao wamekuwa wakitumia sehemu ya fedha katika mambo ya starehe zaidi kuliko kuwajali yatima ili wapate furaha.

Aliongeza kuwa ni vema kuona umuhimu na haja ya kuwasaidia ili wapate faraja hivyo na katika kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake ameona umuhimu kama kijana kutoa sadaka na kusheherekea na watoto ho kwa wa vitu mbalimbali vikiwemo, chumvi, sukari, sabuni na vifaa vya shule.

Mvamba ambaye pia ni rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha Iringa (RUCU)alisema kuwa endapo vijana wengi wakijenga tabia ya kuwatembelea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu itakuwa fursa kwao kujifunza zaidi na kuwa na moyo wa huruma katika kuwasaidia kuliko kupoteza fedha nyingi katika starehe ambazo ni za muda mfupi tofauti na kuwekeza katika watu.

Aidha ameitaka jamii kujitolea kwa dhati kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji, ikiwa pamoja na kuwatembelea ili kujenga upendo kwa makundi maalumu yenye uhitaji kwa lengo la kupunguza changamoto zinazoyakabili makundi hayo.

Kwa upande wake,Sister Helena Kihwele ni msimamizi mkuu wa kituo cha watoto Yatima cha Tosamaganga alisema kituo kina jumla ya watoto 60 ambao hawajafikisha mwezi mmoja hadi miaka sita, na kuwa changamoto kubwa ni walezi kuwasahau watoto mara baada ya kukabidhiwa kituoni hapo.

“Changamoto hii inatusumbua sana maana baadhi ya walezi hawaji kuwasalimia wala kuwachukua watoto sasa tunapata shida wakati wanapotakiwa kurudi nyumbani, maana umri wa mwisho wa kukaa kituoni hapa ni miaka 6,” alisema Kihwele

Alisema kituo kinapokea watoto wasio na mama au wenye mama ambaye ni anatatizo la akili, na kuwa baadhi ya ndugu ndiyo wamekuwa wakiwatelekeza watoto mara tu wanapowafikisha kituoni hapo.

Changamoto nyingine zinazowakabili watoto ni baadhi ya wazazi kushindwa kuwaendeleza kielimu watoto, kwani baadhi ya walezi huwa hawana mwamko wa kuwaendeleza watoto hao, na hivyo kusababisha watoto hao kutoendelea na masomo.
Mwenyekiti wa Serikali za vyuo vikuu vya Kikatoliki chini, Anord Mvamba ambaye pia ni Rais wa Serikalia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha Iringa, (RUCU) akimkabidhi moja vitu mbalimbali mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tosamaganga kilichoko wilaya ya Iringa mkoani Iringa Helena Kihwele wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa mwanzoni mwa ka. (picha na Denis Mlowe)


Hivyo makala VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU

yaani makala yote VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/vijana-watakiwa-kusaidia-watoto-yatima.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU"

Post a Comment