UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI

UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI
kiungo : UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI

soma pia


UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI

Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard amemweleza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kuwa UCSAF imeleta changamoto chanya kwa kampuni za simu za mkononi zinazotoa huduma za mawasiliano nchini
Richard ameyasema hayo wakati wa ziara ya Nditiye ya kukagua changamoto za mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali wilayani Sengerema mkoani Mwanza.  Richard amefafanua kuwa awali kampuni za simu za mkononi nchini zilisita kuwekeza kwenye vijiji mbali mbali ambavyo havina mawasiliano nchini kwa kuwa havina mvuto wa kibiashara ambapo kampuni hizo zilikuwa zinakwenda maeneo ya mijini yenye mvuto wa kibiashara
“Ila sasa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano tunashirikiana na kampuni za simu za mkononi kufikisha huduma za mawasiliano vijijini na kampuni zimepata mwako,” amesema Richard. Ameongeza kuwa Serikali imekuwa inatoa ruzuku kwa kampuni hizo ili waweze kujenga minara kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano
Nditiye amesema kuwa amefanya ziara ya siku tatu ya kukagua mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali wilayani Sengerema ili kuona changamoto za mawasiliano ambapo amekiri uwepo wa changamoto za mawasiliano kwenye Wilaya hiyo kwenye baadhi ya kata ambapo ina jumla ya kata 21 na kubaini uwepo wa ukosefu wa mawasiliano kabisa kwenye baadhi ya maeneo, mawasiliano ya kusuasua na mahitaji ya kuongeza nguvu ya usikivu wa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) akisikiliza kwa makini taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji Kata ya Katwe, Wilaya ya Sengerema, Mwanza, Deus Ngodagula Masasi (aliyenyoosha kidole) kuhusu ukosefu wa mawasiliano kwenye kisiwa cha Maisome wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano wilayani humo. Naibu Katibu Mkuu – Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeshika ramani) akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, UCSAF, Mhandisi Albert Richard (wa kwanza kushoto).
Naibu Katibu Mkuu – Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeinua mkono) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua changamoto ya mawasiliano kisiwani Maisome, Mwanza. Anayesikiliza wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Kilimbe.
Diwani wa Kata ya Bangwe, wilayani Sengerema, Mwanza, Yonas Magikulu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano Wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI

yaani makala yote UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/ucsaf-yaleta-changamoto-chanya-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI"

Post a Comment