"TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE

"TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa "TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : "TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE
kiungo : "TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE

soma pia


"TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE

Mwambawahabari

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka jamii kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu ili kuwa na Jamii yenye mabinti wasomi na kuondokana na ukandamizaji wa watoto wa kike na wanawake.



Dkt. Ndugulile ametoa rai hiyo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati akishirikiana na wananchi katika ujenzi wa Bweni la shule ya Sekondari Mikalanga ambalo kwa kiasi kikubwa wananchi wametoa nguvu zao katika kufanikisha ujenzi huo.



Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa suala la elimu kwa mtoto wa kike na muhimu kutokana na changamoto za mtoto wa kike hasa suala la mimba za utotoni ambazo zinapelekea kupotea kwa ndoto za wanafunzi wa kike wengi.

Naibu Waziri Ndugulile amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo Mtoto mmoja kati ya watoto watatu wa kike hupata mimba za utotoni na kukatisha ndoto za Mtoto wa kike kupata elimu kati ya miaka 15 mpaka 19 ikiwa sawa na asilima 27.

"Tunataka taifa la mabinti waliosoma, madaktari, wahandishi na wataalam wengine tuunge mkono juhudi hizi ili tuondokane na na changamoto zinazopelekea watoto wa kike kupata mimba za utotoni" alisisitiza Dkt. Ndugulile. 

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani amemshukuru Naibu Waziri kwa kuamsha ari na kutoa mchango wake wa mifuko 50 ya Saruji ili kufanikisha watoto wa kike kupata elimu na kuondokana na changamoto za kukosa mabweni inayosababisha watoto wengi kupata mimba. 


Akitoa taarifa ya Mradi kwa niaba ya wananchi mjumbe wa Kamati ya ujenzi wa Bweni hilo Inviolatha Lupogo amesema kuwa hadi kukamilika kwa mradi huo utagharimu kiasi cha Shillingi 139 ambapo mchango wa wananchi unatarajiwa kuwa ni Shillingi Millioni 43 na hadi sasa wananchi wamechangia shillingi Millioni 11


Ameongeza kuwa lengo la mradi huo ni kupunguza adha ya kutembea umbari mrefu , kuwapangisha watoto wa kike kiholela ambapo kwa mwaka 2017/2018 jumla ya watoto wa kike 12 walikatishwa masomo yao sababu ya ujauzito.



Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya  ujenzi wa Bw. Lilbrad Kinunda amesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa Naibu Waziri Ndugulile na kushirikina na wananchi katika ujenzi wa bweni hilo na wao wanaunga mkono juhudi hizo kwa kujitolea  katika kujenga bweni hilo kwa amasa zaidi.


Katika kuuunga mkono juhudi za wananchi wa Mikalanga Naibu Waziri Dkt. Ndugulile alitoa jumla ya mifuko 50 ya saruji na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani amechangia jumla ya mifuko 30 ya saruji.


Hivyo makala "TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE

yaani makala yote "TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala "TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/tunataka-taifa-la-mabinti-wasomi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to ""TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI” DKT.NDUGULILE"

Post a Comment