title : TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE
kiungo : TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE
TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE
Mwambawahabari
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma za maudhui mtandaoni kati ya Machi na Desemba 2018.
Kati ya leseni hizo, 93 ni kwa wamiliki wa blogs, majukwaa ya majadiliano mtandaoni mawili, redio mtandao 32, televisheni mtandao 97.
Kilaba ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) inayofanyika katika ofisi za TCRA jijini Dar es Salaam.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao na kujihakikishia kuwa maudhui yanayotolewa yanakuwa sahihi.
“TCRA haizuii matumizi ya mitandao ya kijamii katika utoaji wa maudhui bali tunalinda maslahi mapana na endelevu ya jamii inayotumia huduma hizo hususani watoto,” amesema Kilaba.
Amesema kutokana na hali hiyo hivi sasa Watanzania wanapata taarifa ya habari bure kupitia chaneli za ndani kwa mujibu wa sheria.
Hatahivyo baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya blog na TV online hawajaridhishwa na gharama kubwa inayotozwa na mamlaka hiyo ambapo hulazimika kulipia milioni moja kila mwaka na kodi nyingine ambayo hulipwa TRA, jambo ambalo ni hasara kwao ukizingatia kuwa hawazalishi kikubwa kiasi hicho, na wameomba serikali kuangalia namna ya kupunguza tozo hizo,ama kutoza kutokana na uwezo wa mtu.
Hivyo makala TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE
yaani makala yote TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/tcra-yasajili-mitandao-224-waendesha.html
0 Response to "TCRA YASAJILI MITANDAO 224, WAENDESHA MITANDAO NAO WAOMBA GHARAMA ZIPUNGUZWE"
Post a Comment