title : TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA
kiungo : TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA
TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA
Wanafunzi 53 kutoka katika Kituo cha Elimu ya Maendeleo ya Afya ( CEDHA) cha Jijini Arusha, walimu na Baadhi ya Wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa hitimisho la mafunzo ya udhibiti na matumizi salama ya vyanzo vya mionzi
Na. Vero Ignatus, Arusha
Tume ya Nguvu za Atomiki nchini imeendesha mafunzo kwa wanafunzi 53 wa kituo cha elimu ya maendeleo ya Afya CEDHA juu ya matumizi ya mionzi
Mafunzo hayo yamefanyika makao makuu ya ofisi ya TAEC iliyopo Jijini Arusha kwa siku tatu yakiwa na lengo la kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo faida, matumizi udhibiti na madhara yatokanayo na mionzi mahala pa kazi pamoja na sheria zake
Mafunzo yameendeshwa na TAEC kupitia wataalamu wake wafuatao
Bw Eng. John Ben Ngatunga - Mtafiti
Bw Simon Mdoe- Mtafiti
Bw Jerome Mwimanzi- Mtafiti
Bw Siwidhani Ndovi- Mtafiti
Kwa mujibu wa TAEC lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya matumizi salama ya vyanzo vya mionzi ili kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo faida, matumizi, udhibiti na sheria zake ili kuwawezesha wanafunzi hao kuelewa matumizi salama ya teknoljia ya Nyuklia na kujilinda pindi watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi hapo.
Peter Ngamilo ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka TAEC ameeleza Kutokana na ufuatiliaji wa Mara kwa mara ambao unaambatana na ukaguzi unaofanywa na TAEC ,mpaka hivi sasa hakuna athari zozote zilizojitokeza kwenye maeneo ya kazi isipokuwa tu kuna baadhi ya vituo vichache ambavyo vimekuwa vikikiuka utaratibu na tayari imeshavichukulia hatua za Kisheria.
Hatua mojawapo iliyochukuliwa na TAEC ni pamoja na kuvifungia ili visitoe huduma ambayo itapelekea kusababisha athari za madhara ya mionzi kwa Wafanyakazi na mazingira yanayozunguka
TAEC inapenda kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali ili kupata elimu hiyo juu ya yanayohusu udhibiti usalama wa mionzi na matumizi sahihi ya teknolojia ya nyuklia hapa nchini
Hivyo makala TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA
yaani makala yote TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/taec-yaendesha-mafunzo-kwa-wanafunzi-wa.html
0 Response to "TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA"
Post a Comment