MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU

MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU
kiungo : MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU

soma pia


MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU

Na Rhoda Ezekiel Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wenye watoto walemavu kuacha kuwaficha ndani na badala yake wahakikishe wanapeleka shule ili wapate elimu kama watoto wengine.

Aidha amewataka wazazi wote waliowahifadhi watoto wao katika kituo cha Watoto wenye ulemavu Kakonko kuwatembelea na kuwapa huduma zinazo stahiki kwa kuwa na wao wanahaki ya kuthaminiwa kama watoto wengine.

Maagizo hayo aliyatoa jana wilayani Kakonko wakati akikabidhi baiskeli saba za watu wenye ulemavu zilitotolewa na Shirika lisilo la kiserikali Help age International linalosaidia wazee na makundi maalumu yenye uhitaji kwaajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu waliokuwa wameshindwa kwenda shule.

Amesema wapo watu wengi wenye ulemavu lakini sasa hivi ni wasomi wakubwa na wanazisaidia familia zao na kulisaidia Taifa, kuwa mlemavu ni jambo la kawaida hivyo wazazi wanatakiwa kuwaibua watoto wengine waweze kupata elimu na sio kuwanyanyapaa.

" Ulemavu sio ugonjwa, leo unaweza kuwa mzima kesho ukapata ajali na bado ukawa mlemavu, hivyo tunatakiwa kuwajali na kuwalinda walemavu bila ubaguzi wowowte kwani hata wao wanahitaji huduma za muhimu kama watu wengine", amesema Kanali Ndagala.

Aidha aliyaomba mashirika mengine ya wakimbizi kuendelea kutoa misaada katika Wilaya hiyo, kwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa na miundombinu mbali mbali ilikusaidia Wilaya hiyo inainuka na kusonga mbele.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Help age Kigoma Fredi Kianda alisema Baiskeli hizo walizozitoa zina thamani ya shilingi milioni tisa na laki nane na hiyo ni hatua ya awali wataendelea kufanya uchunguzi kwa makundi yanayo hitaji msaada ili waweze kuleta msaada.

Amesema awali walianza kwa kutoa magodoro 600 kwa wazee wasio jiweza na shirika hilo litaendelea kutoa misaada hoyo ilikuhakikisha makundi ya walemavu na wasiojiweza wanapata misaada na wanaishi vizuri.

Shirika la help age shirika linalo husika kusaidia wazee na watu wenye mahitaji mbalimbali pamoja na walemavu walifanya uchunguzi na kufanya tathimini na kubaini watoto saba wenye ulemavu wa viungo na kuamua kuleta vifaa kwaajili ya kuwasaidia watoto wanaaandikishwa Shuleni.

Zoezi lingine la kufanya uchunguzi kuendelea kuchunguza wazeee na Watu wenye ulemavu lomezinduliwa rasmi na wataendelea kupita vijijini kuwabaini wote pamoja na watoto wenye ulemavu waliofichwa.


 


Hivyo makala MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU

yaani makala yote MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mkuu-wa-wilaya-kakonko-kanali-ndagala.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU"

Post a Comment