title : SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI
kiungo : SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI
SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI
DAR ES SALAAM, Tanzania - Klabu ya Singida United imepangwa kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Mshindi wa pili wa Ligi Kuu ya Kenya, Bandari FC, katika michuano ya SportPesa Cup inayotarajiwa kutimua vumbi kwa msimu wa tatu mfululizo kuanzia Januari 22-27 katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Ratiba hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, iliwekwa hadharani na waandaaji wa michuano hiyo, kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambapo mabingwa mara 27 wa Tanzania Bara, klabu ya Yanga wataumana na mabingwa wa Ngao ya Jamii ya SportPesa, timu ya Kariobangi Sharks kutoka nchini Kenya majira ya saa 10:15 jioni katika mechi ya pili ya siku ya ufunguzi.
Mabingwa watetezi Gor Mahia wataumana uso kwa uso na Mbao FC kutoka jijini Mwanza siku ya Januari 23 majira ya saa nane kamili mchana huku mtanange wa mwisho kwa hatua ya robo fainali ukipigwa kati ya Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC watakaowavaa AFC Leopards majira ya saa 10:15 jioni.
Mitanange ya nusu fainali itapigwa Januari 25 huku mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ukipigwa Januari 27 majira ya saa 8:00 mchana ambayo ni siku ya mwisho ya mashindano.
Nae Mkurugenzi wa Mashindano (TFF), Salum Madadi amesema maandalizi yote ya shindano yamekamilika, huku akiwataka mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia mechi kali na za kusisimua.
Hivyo makala SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI
yaani makala yote SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/singida-bandari-kufungua-dimba-ratiba.html
0 Response to "SINGIDA, BANDARI KUFUNGUA DIMBA, RATIBA YA SPORTPESA CUP IKIWEKWA HADHARANI"
Post a Comment