SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI.

SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI.
kiungo : SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI.

soma pia


SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI.












Serikali imefuta kodi ya pango la ardhi kwa Taasisi na Madhehebu ya dini nchini kuanzia mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Hatua hiyo imetangazwa jana Jumapili Januari 27, 2019 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi jijini Mbeya wakati wa ibada ya kuwaweka wakfu viongozi wa Jumuiya Kuu ya Kanisa la Kibaptisti Tanzania (BCT).

Lukuvi alisema Rais Magufuli ameiagiza wizara hiyo kutoyatoza kodi madhehebu ya dini kwa sehemu ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya kufanyia ibada.


"Rais ameagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu wa fedha madhehebu ya dini yasilipe kodi ya ardhi kwa maeneo ambayo huduma za maombi na ibada zinatolewa, hata hivyo msamaha huu hauhusu maeneo ambayo kuna miradi ya kuingiza fedha ambayo tunajua madhehebu mengi yameanzisha," alisema Lukuvi.


Lukuvi alifafanua maagizo hayo tayari yametolewa kwa makamishna wa ardhi wa kanda na mikoa pamoja na maofisa ardhi wa majiji, manispaa na halmashauri nchi nzima.


Hata hivyo, Lukuvi ametoa nafasi ya kukutana na viongozi wa dini ambao wana migogoro ya ardhi kwenye maeneo ambayo wanatoa huduma.


"Najua kuna migogoro mingi kwenye maeneo ambayo mnatoa huduma hivyo nawakaribisha ofisini kwangu Dodoma na kama migogoro itakuwa mikubwa nitafika mpaka eneo la mgogoro," alisema Lukuvi.


“Wizara yangu imepewa jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kabla ya mwaka 2020 na tusipotatua migogoro ya dini inaweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini hivyo hatutaki kuifuga migogoro iliyopo,” alisema.


Awali, askofu wa kanisa la Baptisti nchini, Arnold Manase amesema kanisa lake ni moja ya madhehebu yanayoongoza kuwa na migogoro ya ardhi na baadhi ya waumini wa kanisa hilo.


"Kwa kuwa waziri mwenye dhamana upo naomba nafasi nije ofisini kwako nikueleze migogoro iliyopo ndani ya kanisa langu ili uangalie namna ya kuitatua maana migogoro imekithiri mpaka kufikia hatua ya kujenga makundi miongoni mwa waumini," alisema Manase


Hivyo makala SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI.

yaani makala yote SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/serikali-yafuta-kodi-ya-ardhi-taasisi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAFUTA KODI YA ARDHI TAASISI ZA DINI."

Post a Comment