title : SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI
kiungo : SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI
SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI
Na.Khadija seif,Globu ya jamii.
Malkia wa Bongofleva kwa upande wa Tanzania Bara Jamila a.k.a Baby J awataka wasanii wa Bara hasa wanawake kupeana ushirikiano katika kazi ili kuiendelea kuzalisha vipaji kwa wingi hasa kwenye muziki wa bongofleva na kuendelea kukuza tasnia ya muziki .
baby j amesema jina lake linaendelea kutambulika na kung'ara vizuri kimuziki kutokana jitihada ,kuamini kile wanachokifanya pamoja na kujichanganya na kushirikiana na wasanii wengi mbalimbali ili kuendelea kujifunza mambo mengi yahusuyo muziki.
Hata hivyo baby j ameeleza jinsi mitandao ya kijamii ilivo na nguvu kwa Sasa katika kuendesha shughuli za kimuziki na kuutangaza inasaidia kuwapa fursa mashabiki kufahamu upo wapi ,una kazi ipi na unajiandaa na lipi kitendo hiko kimekua kigumu kwake kutokana na kutopenda maisha ya mitandaoni.
" Nitarudi tena kufanya kazi za kimuziki kwani nina kipaji ,muziki ni kilevi changu ila kwa Sasa naendelea na majukumu ya familia hasa kumlea mtoto wangu mpya. "Amesema Baby J
Pia ameeleza kuwa kwa wanamuziki wa Zanzibar wengi hawajiamini katika kile wanachokifanya kutokana na kukatishwa tamaa kwani hata yeye aliyekuwa akisimamia kazi zake alishamkatisha tamaa lakini aliweza kujiamini kwa kuendelea kufanya vizuri kwa upande wa Bara.
Na amemtaja Mwanamuziki Diamond platnum kuwa ni mtu ambae anamshauri na kushirikiana nae vizuri katika kazi za muziki kwani anaamini mchango wake ni mkubwa katika tasnia ya muziki wa Bongofleva.
Hivyo makala SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI
yaani makala yote SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/sababu-zinazofanya-wasanii-wa-kike-wa_19.html
0 Response to "SABABU ZINAZOFANYA WASANII WA KIKE WA TANZANIA BARA KUTOTOBOA KIMUZIKI"
Post a Comment