title : MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU
kiungo : MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU
MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU
MSANII wa filamu nchini Yusuph Mlela amewapongeza waandaji wa tamasha la filamu za kitaifa (SZIFF)kwa kuwapa fursa wasanii kujifunza kupitia masoko ya nje.
Mlela ameeleza hayo leo,kuwa fursa waliyoipata katika mchakato wa tuzo ikiwa wazi kwamba bado wanafanya jitihada katika kuboresha na kukuza tasnia ya filamu nchi hasa kuonyesha filamu za nje na kukutanisha watu wanaofanya vizuri kutoka nchi za nje kutoa elimu kwa wasanii wa nchi zingine.
"Kuna utofauti mkubwa sana ukiangalia filamu za mataifa mengine na za kwetu hasa kwenye mtiririko wa matukio,ubora, uvaaji wa uhusiano , sisi bado tuko nyuma sana". Alisema mlela
Hata hivyo amefafanua kupitia tamasha hilo tasnia itaimarika na kupanuka na kupata masoko ya nje na kujitangaza kwani sanaa ni ya watu wote ni wakati wa wasanii kushirikiana kwa pamoja.
Aidha Mlela amesema kwa mwaka jana filamu ya kesho iliingia sokoni na kufanya vizuri aliyomshirikisha msanii Gabo zigamba na kwa mwaka huu kujipanga na vitu vizuri ambavo viko jikoni na kuwasihi mashabiki wakae mkao wa kushudia vitu vizuri.
Pia ametoa rai kwa waandaji wa Tuzo hizo kufanya kitu cha kipekee na tofauti katika kuboresha na kunogesha msimu huu wa pili japo ni changa kwa sasa , anaamini katika jambo lolote zuri lazima mawazo na maoni ni muhimu kuwasilishwa sehemu husika kufanyiwa ufumbuzi.
Hivyo makala MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU
yaani makala yote MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mlela-awapongeza-waandaji-wa-matamasha.html
0 Response to "MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA MATAMASHA YA FILAMU"
Post a Comment