title : NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA
kiungo : NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA
NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WANAMUZIKI wa dansi wenye uraia wa nchi ya Congo ambao wapo nchini Tanzania wameomba wapatiwe vibali vya uraia kwani wameka nchini kwa muda mrefu.
Wametoa ombi hilo kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaa Paul Makonda ambaye aliamua kukutana na wasanii wa tasnia mbalimbali kuzungmza nao na kusikia changamoto zinazowakabili.
Mwanamuziki maarufu katika muziki wa dansi nchini Nyoshi El-Saadat amesema amekuwa nchini Tanzania kwa miaka 25 sasa lakini bado wanaendelea kusumbuliwa na imefika mahali wanajificha juu ya dali.
“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaomba utusaidie kwenye hili la uraia.Tunaomba tuwe raia wa Tanzania, ni nchi ambayo tumeishi miaka mingi.Mimi nipo Tanzania kwa zaidi ya miaka 25 , nimebahatika kupata watoto 12, sasa leo hii naenda wapi zadi ya kubaki katika nchi nzuri ya Tanzania,”amesema Nyosh-Elsaadat
Kwa upande wake mwanamuziki na mugizaji wa filamu nchini Patcho Mwamba ametoa ombi kwa Makonda la kutaka aangalie namna ya kuwasadia wapate uraia wa Tanzania.
“Tunakuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda utusaidie kwenye hili la uraia.tupo nchini kwa muda mrefu tukiendelea na maisha yetu. “Nikienda Congo nikikaa siku tatu tu au wiki moja narudi nchini Tanzania.Kule Congo tulikuwa tunakula mbwa, hivyo sitaki tena kula mbwa.Tusaidie kwenye suala la uraia mkuu wetu wa mkoa,”amesema Patcho Mwamba.
Wakati huo huo wanamuziki hao wamezungumzia kushuka kwa mapato kutokana na shughuli za muziki kuzuiliwa kwa kupiga mwisho saa sita usiku. Wasema wategemea muziki kuishi na kuendesha maisha yao kupitia muziki wa dansi na wanasomesha watoto pamoja na maisha mengine.
Hivyo makala NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA
yaani makala yote NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/nyoshi-el-saadat-patcho-mwamba-waomba.html
0 Response to "NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA"
Post a Comment