NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI
kiungo : NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

soma pia


NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiangalia na huku akipewa maelezo na Afisa Misitu, John Mtika  kuhusu hatua za miche ya miti ya miembe inavyokua wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea  ofisi za  Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti mkoani Morogoro kwa lengo la kujua imejipangaje kuzalisha miche za miti yenye ubora  ikiwemo ya mbao pamoja na ya  matunda ambayo itasambazwa nchi nzima Kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo, Edgar Masunga pamoja na watumishi wengine.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti, Edgar Masunga pamoja  na Afisa Misitu, John Mtika ( kushoto) mara baada Naibu Waziri huyo alipotembelea bustani za miti mbalimbali katika Kurugenzi ya Uzalishaji Miche ya Miti iliyopo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti, Edgar Masunga, wakati alipokuwa akikagua jana  bustani mbalimbali za miche inayooteshwa na Kurugenzi hiyo mkoani Morogoro, Kulia ni Afisa misitu wa Kurugenzi hiyo, Fandey Mashimba.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akipanda mti ambao upo hatarini kupotea ambapo kwa sasa nchini Tanzania miti ya aina hiyo inapatikana mkoani Lindi pekee
Na.Lusungu Helela - Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameahidi kulifanyia kazi suala la kugawa miche  ya miti bure kwa Wananchi  ili wakaipande iliyooteshwa na Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya miti   kuwa utaratibu huo hauwezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa na Serikali.
Imeelezwa kuwa uzoefu uliopo unaonesha kuwa vitu vingi ambavyo Serikali imekuwa ikivigawa bure kwa Wananchi bila wananchi hao kuchangia gharama yoyote vitu hivyo hushindwa kuthaminiwa.
Mhe. Kanyasu alitoa kauli hiyo jana   mkoani  Morogoro wakati alipotembelea ofisi za  Kurugenzi hiyo kwa lengo la kujua imejipangaje kuzalisha miche za miti yenye ubora  ikiwemo ya mbao pamoja na ya  matunda ambayo itasambazwa nchi nzima.
Alisema utaratibu huo itabidi uangaliwe upya kwa vile ni ngumu kwa wananchi walio wengi kuitunza  kwa sababu hawasikii uchungu na walio wengi hujikuta wakiitupa au kuiacha bila kuimwagilia hadi inakufa.
''Ukichukua miche leo halafu ukaipeleka mkoani Shinyanga ukagawa bure yote italiwa na ng'ombe na vivyo hivyo ukaipeleka Dodoma  yote itakufa kwa vile haitamwagiliwa maji  kwa sababu ni ya bure'' Amesisitiza
 Alisema siku zote kitu cha bure hakithaminiwi, hivyo lazima kila Mwananchi achangie kidogo  lakini isiwe bure kabisa.
Hata hivyo, Mhe. Kanyasu alisema miche ya miti  inaweza kutolewa bure kwa taasisi za umma kama vile shule ila  kwa makubaliano maalumu lakini sio kwa wananchi.
Aidha, Aliitaka Kurugenzi hiyo ijiendeshe kibiashara badala ya kujikita kutoa huduma kwa wananchi
Katika hatua nyingine, Mhe Kanyasu aliiagiza  Kurugenzi hiyo ifungue  utalii wa bustani wa miti na maua  katika jiji la Dodoma ambao ni moja ya aina ya  utalii unaopendwa sana hasa na Wanamazingira.
Alisema miji kama Arusha pamoja na Mwanza imeanzisha utalii huo licha ya kuwa kumekosekana mwongozo wa kuziboresha bustani hizo lakini hata hivyo watalii wengi wamekuwa wakimiminika katika bustani hizo.


Hivyo makala NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-waziri-kanyasu-aonesha-wasi-wasi_31.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI"

Post a Comment