Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu

Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu
kiungo : Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu

soma pia


Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu

 Waziri Ummy Mwalimu baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya siku ya ukoma Duniani ambayo itafanyika kesho akiwakabidhi waathirika wa ukoma chakula kwenye makazi yaliyopo Nunge wilayani Kigamboni.Siku ya ukoma Kitaifa itafanyika kesho makazi ya watu waishio na ukoma Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,,Jinsia Wazee na Watoto akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rachel Mhando,Viongozi wa wizara pamoja na wazee hao wakitoa ujumbe wa kuashiria kuondoa unyanyapaa dhidi ya waathirika wa ukoma.
 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwapa mikono waathirika wa ugonjwa wa mikono wanaoishi makazi ya Nunge wilayani Kigamboni ikiwa ni ishara ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika wa ukoma
 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwapa mikono waathirika wa ugonjwa wa mikono wanaoishi makazi ya Nunge wilayani Kigamboni ikiwa ni ishara ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika wa ukoma

 Waziri Ummy Mwalimu akitoa tamko la siku ya ukoma Duniani ambapo aliwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kuchunguza miili yao pamoja na watoto kama kuna mabaka rangi ya shaba  yasiyo na hisia na kuwahi hospitalini mara waonapo dalili hizo.
 Mwaathirika wa ugonjwa wa Ukoma Vumilia Chambuso akitoa Shukrani kwa Waziri wa Afya,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mara baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Ukoma katika makazi ya Ninge Jijini Dar es Salaam.
 Askari akimuongoza mtuhumiwa anayedaiwa kuuza maeneo katika makazi ya Nunge baada ya kutajwa na mmoja ya mkazi wa makazi ya Nunge. 
Kamishina Msaidizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Rabikila Mushi akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika makazi ya Nunge.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema jamii imekuwa na mtazamo hasi na kufanya wagogonjwa wa ukoma umekuwa kuogopwa na kuweka unyanyapaa na kufanya wagonjwa hao kuogopwa kuwa tegemezi na kutothaminiwa.

Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ambayo hufanyika Jumapili ya mwisho ya Januari iliyofanyika katika makazi ya Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Amesema tunaadhimisha miaka 60 ya uwepo wa Shirika la Ujerumani linaloshughulikia masuala ya Kifua kikuu na Ukoma (GLRA). Shirika hili limekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali kuhakikisha Ukoma unatokomezwa kwa kufadhili shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa vyombo vya usafiri kwa waratibu wa Kifua kikuu na Ukoma nchi nzima.


Ummy Siku ya Ukoma Duniani inatupa fursa ya kutathmini mwelekeo wa jitihada zetu nchini na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu kwa kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni “Tutokomeze Ubaguzi, Unyanyapaa na Chuki dhidi ya Waathirika wa Ukoma.

Aidha amesema waathirika wengi wa Ukoma wananyanyapaliwa na kubaguliwa katika maeneo mengi, takriban asilimia 50 ya wagonjwa wa Ukoma hupatwa na sonona na huishi maisha ya huzuni na wasi wasi mkubwa.

Amsema wadau na wananchi wote wanahimizwa kuungana na kuongeza nguvu katika kupinga matukio vyote vya ubaguzi na unyanyapaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna sheria kandamizi kwa watu walioathirika na ugonjwa wa Ukoma. Kwa kufanya kazi pamoja na kupinga kwa nguvu zote vitendo hivi itatusaidia kupiga hatua mbele kuelekea kutokomeza Ukoma.

Ummu amesema nchi imefikia viwango vya utokomezaji wa Ukoma kitaifa mwaka 2006 kwa kiwango cha chini cha mgonjwa mmoja (1) kati ya watu 10,000, na kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma (NTLP) za mwaka 2017, jumla ya wagonjwa wapya 1,933 waligunduliwa na hivyo kufanya kiwango cha ugunduzi kuwa watu wane (4) kwa kila watu 100,000 na nchi kuwa . miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa Ukoma duniani nchi nyingine ni pamoja na India, Indonesia, Brazil, Ethiopia, Msumbiji, Nigeria na DRC Kongo.

Amesema mikoa 10 iliyogundulika na wagonjwa wapya wa Ukoma wengi zaidi kila mwaka na kuchangia karibia 80% ya wagonjwa wote ni Mikoaya Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro,Pwani,Tanga,Geita,Dodoma,Tabora na Kigoma na Wilaya 20 ambazo hazijafikia lengo la utokomezaji ugonjwa ni Liwale, Lindi vijijini, Nachingwea, Ruangwa, Nanyumbu, Masasi mjini, Pangani, Mkinga, Korogwe, Mvomero, Kilombero, Morogoro vijijini, Ulanga, Shinyanga Manispaa, Mafia, Rufiji, Kilwa, Chato, Nkasi, na Mpanda.

Ametoa rai kwa jamii, wazazi na walezi kuwa sote tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na ya watoto wetu endapo utaona mojawapo ya dalili za Ukoma ambazo ni baka au mabaka mwilini yenye rangi ya shaba na hayana hisia, vijinudu kwenye ngozi au mishipa ya fahamu kuvimba na dalili zingine nyingine ni ganzi kwenye mikono na miguu unashauriwa kwenda kwenye kituo cha tiba kilicho karibu nawe kwa uchunguzi bila kuchelewa.

Ugonjwa wa Ukoma unatibika. Mgonjwa aliyeanza tiba hawezi kuambukiza mtu mwingine na hivyo hakuna sababu ya kumtenga na anaweza kuendelea na shughuli za kawaida za maisha.

"Nachukua nafasi hii kwa niaba ya serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuyashukuru mashirika mbali mbali ya ndani na nje yanayounga mkono juhudi zetu za kutokomeza Ukoma nchini”amesema Ummy


Hivyo makala Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu

yaani makala yote Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mtazamo-hasi-umefanya-wagonjwa-wa-ukoma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu"

Post a Comment