title : Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe
kiungo : Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe
Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe
Mkazi wa Unguja kisiwani Zanzibar Abdulrazak Abdallah, ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi 15m/- katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe.
Abdulrazak ni mmoja kati ya washindi wakubwa watatu wa promosheni ya Tigo Jigiftishe. Wengine ni Emma Kauka mkazi wa Dar es Salaam aliyejishindia shilingi milioni 25 na Sadiki Kilipamwambu mkazi wa Songea alijishindia shilingili milioni 50.
Akipokea zawadi yake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Deogratius David, mshindi huyo alisema zawadi hiyo ya fedha imekuja wakati muafaka kutokana na kuwa anakabiliwa na shida ambazo zinahitaji fedha ili kuweza kuzitatua.“Hii kwangu ni zawadi ya kipekee ambayo Mungu amenipatia kupitia Tigo. Nitatumia sehemu ya fedha kukarabati nyumba ninayoishi ambayo ni kama gofu ili iweze kuwa nyumba kama zilivyo nyumba nyingine. Namshukuru Mungu na Tigo kwa zawadi hii,” alisema
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kwa kanda ya Pwani Deogratias David alisema ni jambo la furaha kuona Promosheni ya Tigo Jigiftishe imekwisha huku ikiwa imeboresha na kubadilisha maisha ya wateja wake.
“Promosheni ya Tigo Jigiftishe imetoa jumla ya shilingi milioni 600 kwa wateja wake. Tunayo furaha kuonna kuwa fedsha hizi zimeweza kuboresha maisha ya wateja wetu,” alisema.Promosheni ya Tigo Jigiftishe ililenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.
Kupitia promosheni hiyo, wateja kumi wa Tigo waliweza kujishindia shilingi milioni moja kila siku, huku mshindi mmoja wa wiki akijishindia shilingi milioni 10 huku washindi wakubwa wakijishindia shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50.
Mshindi wa Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe Abdulrazak Abdallah (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Sh 15m/- kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Deogratias David (wa pili kulia) huku akishangiliwa na baadhi ya wafanyakazi wa Tigo na mtangazaji wa Clouds FM Meena Ally (kushoto) katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jang’ombe kisiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa zawadi ya Sh 15m/- katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe kutoka Zanzibar Abdulrazak Abdallah, akimuonyesha mtangazaji wa Radio Clouds FM Meena Ally hali ya nyumba anayoishi. Mshindi huyo alisema atatumia sehemu ya fedha alizoshinda kukarabati nyumba hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar waliofika katika viwanja vya Jang’ombe kushuhudia mshindi wa zawadi ya Sh 15m/- katika Promosheni ya Tigo Jigiftishe Abdulrazak Abdallah kutoka visiwani humo akikabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyikaa mwishoni mwa wiki.
Hivyo makala Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe
yaani makala yote Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mkazi-wa-zanzibar-aondoka-na-15m-za.html
0 Response to "Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe"
Post a Comment