title : Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi
kiungo : Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi
Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
WIZARA ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) leo Mjini Unguja, imesaini mkataba na Taasisi ya Mifupa MOI. Mkataba huo wa ambao umerasimisha SMZ kuleta wagonjwa wake kupata matibabu katika Taasisi hiyo badala ya kuwapeleka nje ya nchi kama ambavyo imekuwa ikifanyika.
Katika tukio hilo, Utiaji wa saini wa mkataba umefanywa na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Bi. Asha Ali Abdulla pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface huku likishuhudiwa na Mwanasheria wa MOI, Suleiman Mgerwa pamoja na Mwanansheria wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Shufaa Nassoro Ali.
Akizungumza katika tukio hilo, Katibu Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Abdula amesema Serikali ya Zanzibar imeamua kurasimisha ushirikiano na Taasisi ya MOI kwani imekuwa ikitumia gharama kubwa kupeleka wagonjwa nje ya nchi wakati huduma hizo zinapatikana hapa Tanzania.
"Tumekuwa tukipeleka wagonjwa wengi nje ya nchi kwa matibabu hususani hawa wa mifupa, sasa tunafahamu kwamba wenzetu hawa wa MOI wameboresha sana huduma zao hivyo tumeamua wagonjwa wetu waende MOI badala ya kwenda nje, naamnini Mashirikiano hayo haya yatakuwa yenye tija kwa wananchi wetu" alisema bi Asha.
Bi Asha ameongeza kwamba wagonjwa wamekuwa wakienda MOI kupata huduma kwa kipindi kirefu lakini mkataba huu unafanya ushirikiano uwe rasmi na wagonjwa wapokelewe na kupata huduma kwa namna bora zaidi.
" Hili sio jambo jipya, wagonjwa wetu wanakuja huko kupata huduma na tunashukuru kwamba mmekuwa mkiwahudumia vyema, mkataba huu utaboresha namna mnavyowapokea na hata kama kutakuwa na changamoto yoyote kwa mgonjwa tutajadiliana na kuangalia nini cha kufanya kwani mambo sasa yamekuwa rasmi" Alisema Bi Asha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema ni heshma kubwa kwa MOI kuingia mkataba na Wizara ya Afya ya Zanzibar ikiwa ni ishara tosha kwamba Serikali ya Zanziba imetambua maboresho yaliyofanyika MOI pamoja na huduma za ubora wa hali ya juu zinazotolewa.
"Tunawashukuru sana kwa Kuona kwamba huu ni muda muafaka wa kuingia makubaliano nasi, tunawashukuru sana kwa kutambua ubora wa huduma zetu, tunawaahidi kwamba wagonjwa watakaofika kwetu tutahakikisha wanapata huduma bora na kwa wakati kama ambavyo mnatarajia" alisema Dkt Boniface
Dkt Boniface amesema kwamba huduma zinazopatikana MOI kwa sasa ni sawa na zile zinazotolewa katika mataifa yaliyoendelea hivyo wagonjwa kutoka Zanziba watapata huduma nzuri tena kwa wakati.
"Ndugu Katibu Mkuu tumeboresha sana huduma zetu, tuna kitengo cha kisasa cha radiolojia, maabara na wodi za kisasa (Executive ) hivyo tunaamini wagonjwa kutoka Zanziba na watanzania wataendelea kupata huduma bora" Alisema Dkt Boniface
Hatua hii ni itapelekea wagonjwa kutoka Visiwani Zanziba kupata huduma za kibingwa katika Taasisi ya MOI na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kimekuwa kikitumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdulla akikabidhiana mkataba wa Matibabu kwa wagonjwa kutoka Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Bonifece katika Hafla iliyofanyika Zanzibar leo (Picha na MOI)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdulla akitia saini mtaba wa wagonjwa kutoka Zanziba kupata huduma za kibingwa MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitia saini mtaba wa wagonjwa kutoka Zanziba kupata huduma za kibingwa MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani ) katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika Zanziba leo
Mwanasheria wa MOI Bwana Suleimani Mgerwa akitia saini Mkataba huo
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Zanziba Bi Shufaa Nassoro Ali akitia sini Mkataba huo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanziba Bi Asha Ali Abdulla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani ) katika hafla ya utiaji saini leo Zanziba
Hivyo makala Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi
yaani makala yote Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mkataba-kati-ya-serikali-ya-mapinduzi.html
0 Response to "Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi"
Post a Comment