Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19

Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19
kiungo : Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19

soma pia


Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19

TAARIFA KUHUSU KUFANYIKA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI YA MARUDIO MWAKA 2018

Ndugu Viongozi wa Wizara
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ndugu Wananchi, 
Ndugu Walimu na Wanafunzi,
Assalamu Aleykum.

Itakumbukwa kwamba siku ya Jumatatu tarehe 3 Disemba 2018, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ilifuta Mitihani ya Kidato cha Pili kwa wanafunzi wa skuli 189 za Serikali na skuli 60 za binafsi baada ya kugundulika kuwa baadhi ya watu wasiohusika wameipata baadhi ya mitihani kabla ya wakati uliopangwa kufanyika kwa mitihani husika.

Baada ya kufanyika kwa marekebisho yaliyohitajika, Wizara inatangaza rasmi kwamba mitihani ya marudio ya Kidato cha Pili itafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 14 Januari, 2019 na kumalizika tarehe 22 Januari, 2019 kwa wanafunzi wa skuli zote za Serikali na Binafsi za Unguja na Pemba.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inawataka Walimu wakuu wa Skuli zote husika kufanya maandalizi husika ili kuwezesha kufanyika kwa mitihani hiyo katika hali ya utulivu na usalama.

Wizara inatoa shukurani za dhati kwa walimu kwa kuendelea kuwafundisha na kuwashauri wanafunzi wao katika kipindi hiki cha mpito. Aidha, inawashukuru wazazi na jamii kwa jumla kwa kuwa watulivu na kushirikiana na Serikali katika kuona kwamba haki inatendeka kwa wanafunzi wote wa nchi hii.

Wizara inatoa indhari kwamba katika kipindi cha mitihani ya marudio wanafunzi wasiofanya mitihani na wananchi wasipite katika maeneo ya skuli wakati mitihani inaendelea. Aidha Wizara inazuwia kambi za aina yoyote zinazohusiana na mitihani kuanzia Jumatatu ya tarehe 07/01/2019.

Wizara inawatakia kila la kheri wanafunzi wote waliokutwa na kadhia hii na kuwaombea mafanikio katika mitihani hii ya marudio.

Ahsanteni.

Imetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar


Hivyo makala Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19

yaani makala yote Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mitihani-ya-kidato-cha-pili-kurudiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mitihani ya kidato cha Pili kurudiwa kuanzia tarehe 13/01/19"

Post a Comment