MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83.

MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83.
kiungo : MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83.

soma pia


MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Bw. Richard Kayombo Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Waandishi  wa habari wakiwa katika mkutano wa Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Bw. Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 7.99 katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 20I8/20I9  kuanzia Julai hadi Desemba mwaka wa jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Bw. Richard Kayombo, amesema kuwa makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 2.0I ukitofautisha na ukusanyaji wa kipindi hicho kwa mwaka wa fedha wa 20I7/I8.

Bw. Kayombo amesema kuwa katika makusanyo hayo mwezi Desemba mwaka wa jana makusanyo yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huo, kwa TRA  ilikusanya trillioni I.63, huku mwezi novemba  trilioni I.2I, oktoba I.29.

"TRA inawashukuru walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati " amesema Bw. Kayombo.

Katika hatua nyengine Bw. Kayombo ameeleza kuwa katika kutatua kero pamoja na malalamiko ya walipakodi TRA imeweka utaratibu kwa kila siku ya Alhamisi itakuwa ni siku kwa ajili ya mameneja wa mikoa, wilaya kusikiliza na kutatua changamoto za walipakodi.

Amesema kuwa licha ya kutenga siku ya Alhamisi kila kusikiliza kero za walipa kodi, TRA tayari imeanzisha kituo cha ushauri kwa walipakodi kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza ufanisi pamoja na kuwa karibu na walipakodi.

"Tutaendelea kufungua vituo katika mikoa mikoa mingine  ili kuongeza ufanisi katika utendaji" amesema Bw. Kayombo.

Amefafanua kuwa TRA inaendelea kuongeza wigo wa walipakodi kwa kuanza kampeni ya Usajili wa walipakodi wapya kwa kuwapatia namba ya utambulisho ya mlipakodi (TIN) bure katika maeneo yanayofanyika biashara.

Bw. Kayombo amesema kuwa kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo wanatakiwa kuchangamkia fursa ya vitambulisho vya (wamachinga) ambayo vinapatikana nchi nzima katika Ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya kwa shilingi 20,000.

"Vitambulisho vya wamachinga ni maalum kwa wale ambao mauzo yao ghafi hayazidi shilingi 4,000,000 kwa mwaka" amesema Bw. Kayombo.

Hata hivyo Bw. Kayombo wito kwa walipakodi na wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwa ajili ya maendelea ya nchi yetu.










Hivyo makala MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83.

yaani makala yote MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mapato-tra-yaongezeka-asilimia-20i.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAPATO TRA YAONGEZEKA ASILIMIA 2.0I, WAKUSANYA TRILIONI 7.83."

Post a Comment