title : Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru
kiungo : Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru
Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumchukua aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa ili kwenda kuwahoji.
Maombi hayo, yamewasilishwa mahakamani hapo leo Januari 16, 2019 na Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka lakini wakili Swai ameieleza mahakama kuwa mashahidi waliotarajiwa kufika leo wamepata udhuru, ambapo mmoja anaumwa na mwingine amepangiwa kazi Utumishi.
Aidha Swai ameiomba mahakama hiyo amchukue Malinzi na Mwesigwa kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano Takukuru kwa sababu kuna vitu wanataka kuviongezea
Kufuatia hayo, upande wa utetezi wameiomba mahakama ichukulie suala hilo kwa uzito kwa sababu washtakiwa wapo ndani wanateseka.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Mbali ya Malinzi na Mwesigwa, washtakiwa wengine ni Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga, Meneja wa ofisi ya TFF, Miriam Zayumba na Karani Frola Lauya.
ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa na mashtaka 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na USD, 375,418.
Hivyo makala Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru
yaani makala yote Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/malinzi-mwesigwa-waitwa-tena-takukuru.html
0 Response to "Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru"
Post a Comment