title : MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA
kiungo : MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA
MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewapa mbinu wanamuziki Nyoshi El-Saadat na Patcho Mwamba namna ya kufanya ili wawe raia wa Tanzania.
Makonda ametoa kauli hiyo leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam baada ya wanamuziki hao kutoa ombi mbele yake kuwa wanaomba kuwa raia wa Tanzania kwani wamekaa muda mrefu.
Amesema amesikia ombi la wanamuziki hao lakini ili waweze kuupata uraia ni vema wakaandika maombi maalumu kwenye baruana kisha kuiwasilisha katika mamlaka husika ili kuondokana na changamoto ya kuishi maisha ya kujificha.
“Niwaombe wanamuziki Nyoshi El-Saadat na Patcho Mwamba andekeni barua kwa kutaja majina yenu, mnakoishi na kazi ambayo mnafanya kisha leteni.Mkifanya ivyo itakuwa rahisi kupata uhalali wa maombi yenu kushughulikiwa.
“Mnapoishi kwa kujificha maana yake msababisha hata watoto wenu nao kuishi kwa kujificha jambo ambalo kwangu naona si nzuri sana.Andikeni barua ambayo itaweka kila kitu kuhusu ninyi,naamini mtafanikiwa tu,”amesema Makonda.
Kabla ya Makonda kutoa maelekezo hayo kwa wanamuziki hao ambao ni raia wa Congo lakini wamekuwepo nchini Tanzania kwa muda mrefu, waliamua kutoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa huo kuwa wapo nchini kwa miaka mingi lakini changamoto kubwa iliyopo ni aina ya maisha ya kujifichaficha ambayo wanaishi.
Hivyo makala MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA
yaani makala yote MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/makonda-bwanaawapa-mbinu-nyosh-el.html
0 Response to "MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA"
Post a Comment