title : MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO.
kiungo : MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO.
MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO.
MADIWANI wa Manispaa ya Kigamboni wameitaka manispaa ya kigamboni kubuni vyanzo vipya vya Mapato kutokana na vyanzo ambavyo Manispaa hiyo ilikuwa ikivitegemea kuchukuliwa na serikali kuu ,jambo ambalo limesababisha baadhi ya miradi kushindwa kutekelezwa.
Madiwani hao wakichangia katika kikao cha baraza la madiwani wamesema taarifa zao zimekuwa zikijirudiarudia kila mwaka kutokana baadhi ya mambo kutotekelezwa hivyo kulazimu kuandikwa upya .
“Kipindi cha mvua kinaanza muda simrefu namvua zinapo nyesha kichangachui mfereji pale hospitali ,Mahakamani maji yanajaa sijajua mpaka sasa ufumbuzi wake ukoje , na pia pale stand ya Kigamboni kumekuwa na mrundikano wa magari , nini mbadala wake na taa hazija wekwa, haya yote nimekuwa nikiyaulizia kila kikao lakini hakuna utekelezaji “Alisema Dotto Msawa . Diwani wa kakata ya Kigamboni.
Kwa upande wake Mkurugezi wa Manispaa ya Kigamboni Ludigija Ng’wilabuzu ,amesema kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiibuka kama dharua nje ya bajeti ikiwemo ujenzi wa madarasa na madawati na kuwataka Madiwani kuwa wavumilivu na kwamba kila changamoto itatatuliwa kwa wakati wake kutokana na upatikanaji wa fedha.
Kutokana na hali hiyo Madiwani Isaya Mwita, wa kata ya vijibweni na Sanya Bunaya, wa kata ya Kimbiji wakitoa mawazo yao kuhusu uanzishwaji vyanzo vipya vya mapato wameitaka Manispaa kujenga soko la samaki eneo la fery ,kujenga machinjio ,kujenga majengo ya kitegauchumi (shopping mal) kuweka vizuizi na kuanza kutoza watu wanaochimba na kusafirisha mchanga ,kokoto na vifusi.
Hata vyo, Diwani wa kata ya Kisarawe two Issa Hemedi Zahoro ,amepongeza hatua ya Rais John Pombe Magufuli , kuchukua baadhi ya vyanzo hivyo na kufafanua kuwa kunafaida kubwa wanaipata kwani wanajengewa Barabara , masoko ,Hospitali.
“Miradi hii inayotekelezwa na serikali kuu thamani yake ni kubwa inge achiwa Manispaa yetu isingeweza, hata kama tunge achiwa hiyo vyanzo tunavyo lalamikia, nampongeza sana Rais, maana halmashauri hizi zilijisahau sana zilikuwa zinafuja mapato, bora alivyo chukua tujifunze natusipoangalia na kuwa wabunifu halmashauri zitavunjwa”Alisema Zahoro.
Hivyo makala MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO.
yaani makala yote MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/madiwani-kigamboni-waitaka-manispaa.html
0 Response to "MADIWANI KIGAMBONI WAITAKA MANISPAA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO."
Post a Comment