title : MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA
kiungo : MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA
MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA
Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya Watalaam wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa maandalizi ya Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika tarehe 30 Januari 2019 jijini Arusha.
Mkutano huu utafuatiwa na ule wa Makatibu Wakuu tarehe 29 Januari 2019. Pamoja na mambo mengine mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri utapitia na kujadili agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo; taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na masuala ya utawala na fedha.
Mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 1 Februari 2019. Kulia ni Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii na kushoto ni Bw. Bernard Haule, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 28 Januari 2019
Wajumbe kutoka Burundi wakifuatilia mkutano huo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwuliofanyika jijini Arusha tarehe 28 Januari 2019 ngazi ya wataalam
Wajumbe kutoka Kenya nao wakifuatilia mkutano wa wataalam
Wajumbe kutoka Uganda wakiwa kwenye mkutano
Wajumbe kutoka Tanzania nao wakifuatilia mkutano huo
Wajumbe wengine kutoka Tanzania nao wakifuatilia mkutano
Wajumbe wa Tanzania kutoka Wizara, Taasisi na Sekta mbalimbali wakishiriki mkutano kwa ngazi ya wataalam
Hivyo makala MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA
yaani makala yote MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/maandalizi-ya-mkutano-wa-wakuu-wa-nchi.html
0 Response to "MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA"
Post a Comment