title : LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA
kiungo : LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA
LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA
Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kupitia mpango wake wa kuwezesha umilikishaji Ardhi(TLSP) imetoa mafunzo kwa mabaraza ya ardhi ya Vijiji 56 vilivyopo katika wilaya za Ulanga ,Kilombero na Malinyi Mkoani Morogoro ili kukabiliana na migogoro ya ardhi na namna bora ya kuisuruhisha.
Mratibu wa mafunzo hayo JAMES BALELE amesema utafiti uliofanywa na mradi huo umebaini migogoro mingi ya ardhi imekuwa haimaliziki kutokana na uelewa mdogo wa wasuluishi,ufinyu wa vitendea kazi pamoja na miongozo ya kisheria.
Awali akifunga mafunzo hayo ,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga, FADHILI FURAHA ameishukuru wizara ya Ardhi kupitia mpango wake wa uwezeshwaji na umilikishaji Ardhi TLSP kwa kutoa mafunzo hayo yatakayo punguza migogoro kwa wananchi huku mwanasheria wa halmashauri hiyo DEVOTA KISEMBO akaeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo mabaraza hayo ya ardhi.
Mafunzo kwa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji katika Wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Mavimba yakiendelea ikiwa ni sehemu ya hafla ya kuhitimisha mafunzo haya kwa wajumbe wa mabaraza wilayani humo.


Mmoja wa wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kijiji akichangia hoja mara baada ya mgeni rasmi kuwasili katika hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya mabaraza ya ardhi ya kijiji Ulanga.

Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Hivyo makala LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA
yaani makala yote LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/ltsp-yatoa-mafunzo-kwa-mabaraza-ya.html
0 Response to "LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA"
Post a Comment