KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15

KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15
kiungo : KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15

soma pia


KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Simba hadi January 15, 2019 kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo.

Vigogo  wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni pamoja na Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (ambaye hakufika Mahakamani),  Makamu  wake,  Geofrey Nyange maarufu kama 'Kaburu' na Mwenyekiti wa  Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kuwa shauri hilo liliititwa kwa ajili ya kusikilizwa na Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Thomas Simba hayupo.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi January 15,2019.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

Katika shitaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, anadaiwa Machi 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni, jijini Dar es Salaam alijipatia Dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka katika Timu ya Simba wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Katika shitaka la kughushi linawakabili washtakiwa wote, ambapo wanadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh. Milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika shtaka jingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya March10 na September 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.



Hivyo makala KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15

yaani makala yote KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kesi-ya-vigogo-simba-kuendelea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15"

Post a Comment