title : DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA
kiungo : DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA
DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kupitia mikakati iliyopo wamefanikiwa kuchimba zaidi ya 210.
Akizungumza leo na Michuzi Blog, Homera amesema mikakati ya Wilaya ya Namtumbo ni kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kwake yeye maji safi na salama ni kipaumbele chake namba mbili ni maji.
Amefafanua kutokana na malengo ambayo wamejiwekea wamefanikiwa kuchimba visima hivyo 210 ambavyo kwa sehemu kubwa vimechimbwa kwa ufadhili wa wadau mbalimbali wakiwamo Alfridaus na Istiqaama waliochimba visima 106 vifupi.
Pia amesema Anglican chini ya mradi wa boresha afya ya mama na mtoto wamechimba visima 25,kupitia mapato ya ndani wamechimba visima viwili, Help for Underderserved community wamechimba visima 57 na Mei mwaka huu wa 2019 kunatarajiwa kuchimbwa visima virefu 60 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini 60 na visima zaidi ya 40 vitachimbwa Jimbo la Tunduru Kusini.
Ameongeza kuwa kisima kimoja kimechimbwa chini ya ufadhili wa Kanisa Katoliki Parokia ya Namiungo na wanaendelea na uchimbaji kwa kata nzima, pia visima 20 kati ya 25 vimejengwa upya kwa fedha za Serikali chini ya program ya lipa kwa matokeo.
"Tumeamua kutatua changamoto ya uhaba wa maji ndani ya wilaya yetu, kupitia mipango sahihi ya Serikali ya kutatua changamoto za wananchi pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo, leo hii tunajivunia kwani tumeanza vizuri kwenye hili la upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuchimba visima na kazi hiyo inaendelea,"amesema Homera.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,Mh.Juma Homera akiwa sambamba na wananchi wake wakishuhudia kukamilia kwa Kisima cha maji kijiji cha pacha nne kata ya Namiungo kilichochimbwa kwa ufadhili wa Roman catholic Parokia ya Namiungo.Mh Homera amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kupitia mikakati iliyopo wamefanikiwa kuchimba zaidi ya 210.
DC Homera akimtwisha Ndoo ya maji na kumtua Mwenyekiti wa kijiji hicho cha pachanne.
DC Homera akikabidhi kisima kwa wananchi ,ambapo amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kutatua changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kupitia mikakati iliyopo wamefanikiwa kuchimba zaidi ya 210.
DC Homera akiwashukuru wataalamu wakiwa sambamba na mitambo inayotumika kuchimbia visima vya maji, ambayo ni ya shirika lisilo la kiserikali la Marekani 'Help for Underderserved community (HUC) ',ambao mpaka sasa wamechimba visima zaidi ya 57 awamu ya kwanza,bado awamu ya pili Mei mwaka huu 2019 wanatarajia kukamilisha kuchimba visima 100.
Baadhi ya Wananchi wakichota maji kwa miongoni mwa visima vilivyochimbwa na Alfirdaus na Istiqama kijiji cha mchekeni kata ya marumba wilayani Tunduru

Hivyo makala DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA
yaani makala yote DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dc-homera-aweka-mkakati-kutatua.html
0 Response to "DC HOMERA AWEKA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI TUNDURU,VISIMA 210 VYAKAMILIKA"
Post a Comment