title : AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI
kiungo : AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI
AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI
Na Jeshi la Polisi.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imelipongeza Jeshi la Polisi kwa ushirikiano mkubwa wanaoipatia katika suala zima la ulinzi wa raia na mali zao jambo ambalo linawezesha kampuni ya Airtel kuendelea kutoa huduma kwa watanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso alitoa shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro na Mkoa wa kipolisi Kinondoni kwa kusaidia kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahalifu waliotaka kuiba fedha zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka kampuni simu ya Airtel.
Aliongeza kuwa Kampuni yake itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mawasiliano ili wananchi waendelee kupata huduma ya ulinzi na usalama.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso kwa kuleta mrejesho wa kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi na kuongeza kuwa ni watu wachache wanaokuwa tayari kuleta mrejesho wa kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi.
Vilevile, IGP Sirro aliwataka maofisa wote wa Polisi kuiga mfano wa Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Kindondoni ili kujenga na kulinda taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kwa kuwa kazi yao ni kuhakikisha wahalifu wote wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso pamoja na maofisa wa kampuni hiyo walipofika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa lengo la kutoa shukrani na pongezi kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kufanikisha kuwakamata wahalifu waliotaka kuiba zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka Airtel.
( Picha na Jeshi la Polisi.)
Hivyo makala AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI
yaani makala yote AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/airtel-kuendelea-kushikiana-na-jeshi-la.html
0 Response to "AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI"
Post a Comment