title : WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA
kiungo : WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA
WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA
Na Stahmil Mohamed
Dawasa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kufanikisha malengo ya miradi kama ilivyopangwa na serikali ili kufanikisha malengo iliyojipangia.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa alipokuwa katika ziara yake ya kukagua maeneo mbalimbali yanayojengwa miradi ya maji iliyoanzishwa ikiwemo Kimara Bonyokwa,Kinzudi ,Salasala na Saranga ambako amebaini chamgamoto mbalimbali zinazosababishwa na wafanyakazi wenyewe wa Dawasa ikiwemo kuchelewesha kufungia wateja mabomba,kuandikisha wateja hewa pamoja na,kuwalipisha gharama zisizostahili
Hata hivyo Prof Mbarawa amemtaka Meneja mradi Mhandisi Ramadhani Mtindasi kushughulikia dosari zilizojitokeza kwa muda wa siku tatu na ikiwa hajatekeleza maagizo yake atawasimamisha kazi kutokana na uzembe wa kuwacheleweshea wananchi huduma.
Pia Professa Mbarawa amewataka wananchi kutoa taarifa mara moja iwapo watatakiwa kulipa gharama kwani huduma ya ufungaji mabomba ni bure .Professa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wahandisi katika maeneo yote yanayochimbwa mitaro kwa ajiri ya kupitisha mabomba kutowawekea vikwazo ili mradi ukamilike kwa wakati.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha mabomba wakati alipokagua maeneo ya mradi wa maji Kimara Bonyokwa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya mabomba yanayotumika katika mradi huo.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akikagua maeneo mbalimbali katika mradi wa maji unaoendelea Kimara Bonyokwa.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akiangalia mabomba hayo.
Moja ya matenki ya kuhifadhia maji yaliyojengwa katika mradi huo.
Hivyo makala WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA
yaani makala yote WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/waziri-mbarawa-akagua-mradi-wa-maji.html
0 Response to "WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA"
Post a Comment