Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote

Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote
kiungo : Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote

soma pia


Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote

Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaagiza Wakurugenzi wa Bodi za Mazao kuanza mara moja zoezi la kuwatambua na kuwasajili wakulima wa mazao yote nchini lengo likiwa kuwatambua ili kupanga mipango sahihi yenye kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yote.

Ametoa agizo hilo jana tarehe 29 Disemba 2018 wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Mhe. Hasunga amesema ili kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya kilimo na kuandaa mipango madhubuti ya kuendeleza mazao yote ni vyema kuwatambua Wakulima wote nchini na kuongeza kuwa Wakulima wa zao la korosho wametoa funzo kubwa kwa Wizara yake kufanya jambo kama hili katika mazao mengine hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa wiki tatu zilizopita, Waziri Hasunga alitoa agizo kwa Bodi ya Korosho agizo kuandaa daftali maalumu la kuwatambua Wakulima wa korosho kote nchi ambapo moja ya taarifa ambazo zitajumuishwa katika daftali hilo ni pamoja na Jina Kamili la Mkulima, Mkoa, Wilaya, Kata na Tarafa anayotoka.Mambo mengine ni pamoja na Kitongoji, Mtaa au Jina la Kijijini anapotoka, mahali lilipo shamba pamoja na ukubwa wa shamba lake.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa mipango sahihi ya kuwaendeleza Wakulima kuanzia kwenye kilimo chenyewe hadi kufikia katika hatua ya kuvuna, kuhifadhi na kulifikia soko ni vyema kuwa na mfumo maalumu wa kanzi data (Database) ya kuwafahamu ili kushughulikia mahitaji yao kisasa na kwa haraka zaidi.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akifatilia mkutano wa Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, uliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018.
Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao,  wakifatilia mkutano wa kazi ulioongozwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018.



Hivyo makala Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote

yaani makala yote Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/waziri-hasunga-aziagiza-bodi-za-mazao.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote"

Post a Comment