Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili

Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili
kiungo : Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili

soma pia


Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili

Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA ) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi, sheria na kanuni zinazosimamia utumishi wa umma ili kufikia malengo yakutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge kama dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inavyoelekeza.

Akizungumza  kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa OSHA, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema kuwa kikao hicho ni fursa pekee ya kutathmini utendaji wa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuboresha ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Baraza hili la Wafanyakazi linasisitiza umuhimu wa watumishi kufanya kazi kwa maadili na nidhamu ya hali ya juu kama wakaguzi wa masuala ya Afya na Usalama  katika maeneo ya kazi ili muweze kuwa mfano wa kuigwa na Taasisi nyingine za Umma zinazofanya kazi zinazoshabihiana na za kwenu.”

Akifafanua Bw. Kajugusi  amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati, kuondoa uzembe, ubadhirifu pamoja na vitendo vyovyote vya rushwa mahala pa kazi, ikiwa ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuongeza tija. Aliwaasa watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwa kuzingatia malengo yaliyopangwa kwa wakati husika ili kuchochea maendeleo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, akizungumza  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, akimkaribisha  Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Andrew Massawe, Jijini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) kinachofanyika  Jijini  Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
                                                          


Hivyo makala Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili

yaani makala yote Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/watumishi-osha-waaswa-kufanya-kazi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili"

Post a Comment