title : Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu
kiungo : Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu
Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kila mwaka kuna wahitimu wengi ambao wanaingia katika soko la ajira lakini hakuna matokeo ya kazi wanazozifanya. Hayo aliyasema Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji wakati wa mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Amesema ripoti ya Tanzania katika kuandaa rasimali watu iko chini ya asilimia 62 ya viwango vya Dunia ambapo Tanzania imefikia asilimia 53 kufikia huko kumetokana na watu kukosa ubunifu na ujuzi. Dkt. Kijaji amesema kuwa katika viwango na ujuzi na ubunifu kwa viwango vilivyowekwa ni asilimia 50 ambapo Tanzania imefikia asilimia 40 hivyo wasomi lazima kuondoa hali hiyo.
Amesema kuwa mikopo Chechefu kupanda kwake kumetokana na wataalam wa fedha ambapo wamepandisha kutoka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 10 na kuendelea. "Mikopo Chechefu kupanda hakujanywa na mashine bali ni sisi wenyewe ni kazi kwetu wa wataalam wa fedha kutafakari katika kusaidia maendeleo ya Taifa"amesema Dkt.Kijaji.
Hata hivyo amekipongeza Chuo katika ujenzi wa Chuo katika makao makuu jijini Dodoma na kutaka wajenge kwa kutumia wabia na sio serikali kutoa fedha. Nae Mkuu wa Chuo hicho Dkt Tadeo Sata amesema kuwa cho kina changamoto ya walimu pamoja na kuwa na eneo la dogo. Amesema kuwa wanatarajia kujenga Chuo cha Biashara katika eneo la Nara jijini Dodoma katika kuwasogezea huduma wafanyakazi wa serikali. Aidha amesema kuwa Chuo kimeendelea kuwa na ushirikiano na wadau katika utaoaji wa elimu bora.
Naibu Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Tadeo Sata akitoa taarifa ya Chuo katika mahafali 44 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM wakiwa katika mahafali ya 44 yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mahafali ya 44 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya uzamili wakiwa katika mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Hivyo makala Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu
yaani makala yote Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wasomi-waaswa-kuleta-matokeo-cha-chanya.html
0 Response to "Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu"
Post a Comment