title : WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA
kiungo : WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA
WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA
Na Sixmund J. Begashe
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi, amesema Mkoa wa Singida unatarajia kuwa wa mfano nchini kwa upande wa maendeleo yatakayo letwa na wafanya biasha wadogo wadogo wajulikanao kama wa Machinga.
Mh Nchimbi ameyasema hayo kwenye shughuli ya kuwatunuku vyeti vya mafunzo ya MKURABITA pamoja na kukabidhi vitambulisho vilivyo tolewa na Mh Rais Dr Magufuli kwa wafanya biasha wadogo zaidi ya mia sita walio udhuria mafunzo maalumu ya ujasiria mali yaliyoendeshwa na Taasisi ya MKURABITA Mkoani Singida.
Katika zoezi hilo Dr Nchimbi aliwaeleza wajasiria mali hao kuwa Vitambulisho hivyo ni ishara tosha kuwa Mh Rais Magufuli anaupendo mkubwa dhidi ya watanzania wote hasa wananchi wenye vipato vya chini na walie wanyonge hivyo ipo haja kubwa kwa wamachinga nao kuonesha kupokea heshma hiyo kwa kufanya kazi kwa bidi ili waje kuwa wafanya biasha wakubwa na walipa kodi wazuri.
" Heshma aliyotupa Mh Rais Dr John Pombe Magufuli sisi Mkoa wa Singida kupitia ninyi wafanya biasha wadogo wadogo ni kubwa sana, hivyo tunapashwa kuitendea haki heshma hii kwa kuhakikisha tunafanya biashara zetu kwa weledi mkubwa na juhudi ili tupande na kuwa wafanya biashara watakao lipa kodi kwa maendeleo zaidi ya Mkoa wetu na nchi kwa ujumla."Dr Nchimbi alisema
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akionesha mwonekano wa vitambulisho vilivyo tolewa na Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida, pembeni yake ni Meneja wa TRA Mkoa wa Singida Bw Apili Mbaruku.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akiwakabidhi vitambulisho maalumu vilivyo tolewa na Mh Rais Magufuli kwa wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida.
Baadhi ya wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkua wa Singida Dr Rehema Nchimbi (ayupo pichani)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA
yaani makala yote WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wamachinga-kubadili-sura-ya-mkoa-wa.html
0 Response to "WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA"
Post a Comment