title : Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu
kiungo : Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu
Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa kata mbili utakaofanyika tarehe 19 Januari 2019 sanjari na uchaguzi mdogo wa Jimbo la Temeke na Kata 46 za Tanzania Bara uliotangazwa awali.
Akitoa taarifa kwa umma Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne), Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji (Rufaa) Mbarouk Salim Mbarouk amezitaja kata hizo kuwa ni pamoja na Mwanahina iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Shinyanga na Kata ya Biturana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.
“Fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 21 hadi tarehe 27, Disemba mwaka huu. Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 27, Disemba mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 28, Disemba mwaka huu hadi tarehe 18 Januari 2019 na Siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 19 Januari 2019,” alisema Jaji Mbarouk.
Jaji Mbarouk aliongeza kwamba Uchaguzi wa Kata hizo ambao unafanyika kutokana na kujiuzulu uanachama kwa madiwani waliokuwepo awali utafanyika pamoja na uchaguzi wa Jimbo la Temeke na Kata 46 za Tanzania Bara, kama ilivyotangazwa hapo awali.
Akitoa wito kwa vyama vya siasa, Jaji Mbarouk alisema “Tume inapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo”.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu
yaani makala yote Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tume-yatangaza-uchaguzi-mdogo-katika.html
0 Response to "Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu"
Post a Comment