title : WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI
kiungo : WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI
WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI
NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wa Pamba wilayani Igunga wameagizwa kuhakikisha wanasafisha na kuondoa vichaka na magugu yaliyopo kando kando mwa mashamba yao ili kuhakikisha panya na wadudu waharibifu hawageuzi maeneo hayo kuwa maficho na kuingia mashambani kwa ajili ya kula mbegu zilizopandwa.
Kauli hiyo imetolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiwa katika ziara yake ya kuelimisha na kuhamasisha wakulima wa zao la pamba kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo baada ya baadhi ya wakulima kudai uwepo wa panya wanaoshambulia mbegu za pamba walizopanda.
Alisema wadudu na panya ambao wameanza kuingia katika mashamba ya wakulima na kushambulia mbegu ambazo wamepanda wanatokea katika vichaka vichaka vilivyoachwa kando kando ya mashamba hayo. Mwanri alisema wakati juhudi za kuwasiliana Wizara ya Kilimo ili kupata dawa ya kuwaangamiza panya na wadudu hao wanaoshambulia mbegu zilizopandwa ni vema wakulima wakahakikisha mashamba yao ni masafi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa elimu ya kanuni 10 za kilimo bora cha pamba jana katika Kijiji cha Kitangile wilayani Igunga. Kijiji hicho ndio mara ya kwanza kinaanza kulima zao hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa elimu ya kanuni 10 za kilimo bora cha pamba na umuhimu wa kung'oa maotea ya msimu uliopita jana katika Kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akionyesha baadhi ya maotea yaliyokutwa katika shamba la mmoja wa wakulima wakati akitoa maelezo juu ya kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo jana katika Kijiji cha Mbutu wilayani Igunga.
.Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Choma cha Nkola wilayani Igunga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha ) wakati akitoa maelezo juu ya kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo jana wilayani Igunga ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha kilimo cha pamba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI
yaani makala yote WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wakulima-wa-pamba-igunga-waagizwa.html
0 Response to "WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA WAAGIZWA KUONDOA VICHAKA VINAVYOKARIBISHA PANYA MASHAMBANI"
Post a Comment