title : WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA
kiungo : WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA
WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA
Mwambawahabari

NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wilayani Nzega wametakiwa kutumia mbolea aina ya samadi ya ng’ombe wakati wa upandaji wa mazao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo pamba ili kuwa na malighafi za wingi za viwanda
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akitoa elimu ya kuzingatia Sheria na Kununi 10 za kilimo cha pamba wilayani Nzega
Alisema kilimo kinachoendelea wilayani humo kwa wakulima wengi kulima bila kutumia mbolea wala samadi hakitawasaidia wakulima wa Wilaya ya Nzega kuwa na ziada ya kuwasaidia kusonga mbele. Mkuu huyo wa Mkoa alisema samadi itasaidia kurudisha uhai wa ardhi yao ambayo imeanza kuchoka na pia itasaidia kutunza unyenyevu wakati wa ukame na hivyo kumwezesha mkulima kuwa na uhakika wa mavuno mazuri.
Mwanri alisema wawezekaji wanahitaji kuweka mitaji yao sehemu ambayo wanakuwa na uhakika wa malighafi za kutosha kuendesha viwanda vyao wakati wote na sio kwa kipindi kifupi.Aliongeza kuwa ziada ndio itawasaidia kupata ziada ya kuwauzia wawekezaji na hivyo kuwa fedha kwa ajili ya kuboresha maisha yao ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa, kula vizuri, kupata matibabu mazuri na kusomesha watoto wao.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa alisema Ofisi yake kwa kushirikiana na Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Pamba Mkoani Tabora Ingembensabo wanaendelea na mpango wa kutafuta Matreka kwa ajili ya kuvikopesha Vyama vya Ushirika Vya Msingi ili kuongeza ukubwa wa eneo la ulimaji wa zao la pamba na mazao mengine.
Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa kilimo Mkoani Tabora cha pamba na mazao mengine kinakuwa cha kisasa na chenye kuzalisha mazao mengi ambayo yanatoa ziada.Kwa upande wake Ofisa Kilimo Mkoa wa Tabora Modest Kaijage aliwataka wakulima Mkoani humo kuzingatia kanuni za kilimo bora ikiwemo kupanda kwa kutumia mbolea, upandaji mazao kuzingatia vipimo vya zao husika na kufuata mistari.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuwa na idadi ya miche (crop population) inayotakiwa kitaalamu katika shamba na hivyo kuwa na uzalishaji wenye tija unaolingana na ukubwa wa eneo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akitoa elimu ya Sheria ya Pamba
na kununi 10 za zao pamba na unyunyuziaji dawa za kuua wadudu kwenye
eneo la Nzega Ndogo jana.
Hivyo makala WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA
yaani makala yote WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wakulima-tumieni-mbolea-ya-samadi_24.html
0 Response to "WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA"
Post a Comment