title : WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR
kiungo : WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR
WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Zanzibar wamesema CCM itaendelea kuisimamia Serikali ikusanye kwa wingi mapato bila kuruhusu uvujaji wa rasilimali fedha. Wamebainisha kuwa hatua hiyo itasaidia nchi kujitegemea na kuondokana na mfumo wa kutegemea baadhi ya fedha za wadau wa maendeleo zenye masharti yanayokwenda kinyume na Ustawi wa kijamii na Utamaduni wa wananchi wa Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe hao, Mjumbe wa NEC Ndugu Amini Salmin Amour huko katika Kituo cha ufugaji wa Kasa Mnarani Nungwi, ameeleza kwamba endapo Serikali itazidisha kasi ya usimamizi na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato Zanzibar itakuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa. Ndugu Amini ameeleza kwamba Sekta ya Utalii ni moja ya Taasisi muhimu zinazochangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia fedha za kigeni.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Sekta ya Utalii na maeneo ya Uwekezaji kwa lengo la kushauri na kutoa maelekezo kwa baadhi ya sehemu zenye changamoto za kiutendaji. Aliipongeza Kamisheni ya Utalii Zanzibar kwa utendaji wao mzuri uliochangia kuimarika kwa taasisi hiyo na kufanikiwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa Ilani ya CCM.
Pamoja na hayo aliwasihi wananchi kuendeleza Utamaduni wa kufanya Utalii wa ndani ili wajionee vivutio mbali mbali vya utalii vilivyopo nchini pamoja na kufahamu historia na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa kupitia Sekta ya Utalii nchini.
BAADHI ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakisoma machapisho mbalimbali yanayotolewa na Kamisheni ya Utalii hapo katika Kituo cha mawasiliano, Utafiti na Takwimu cha Kamisheni ya Utalii Zanzibar kilichopo Uwanja wa Ndege wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Zanzibar.
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakipatiwa maelezo juu ya huduma zinazopatikana katika ukumbi wa mikutano wa Holeli ya Kimataifa ya Verde iliyopo Mtoni Marine Unguja, katika ziara yao ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakikagua boti na vifaa vya kisasa vilivyopo katika Hoteli ya Kimataifa ya Verde huko Mtoni Marine Zanzibar.
MKURUGENZI Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Miraji Ussi akitoa maelezo ya ramani ya ujenzi wa mradi mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika eneo la Makumbusho ya Kihistoria la Bihole lililopo Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakipatiwa maelezo juu ya Mradi wa Ufugaji wa Kasa uko Mnarani Nungwi, ambapo ni sehemu ya mradi unaoendeshwa na wananchi wakishirikiana na kamisheni ya Utalii Zanzibar.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR
yaani makala yote WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wajumbe-wa-nec-waridhishwa-na.html
0 Response to "WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR"
Post a Comment