title : WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO
kiungo : WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO
WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO
Baraza la watoto la Taifa leo limepata uongozi mpya baada kukamilisha uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Baraza hilo na pia uchaguzi wa Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu na Mweka hazina wa Baraza hilo uchaguzi uliofanyika jana katika Manispaa ya Singida.
Akiongea mara baada ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi huo Mwenyeliti wa Uchaguzi wa Baraza hilo Bi. Joyce Mugambi amewataka viongozi wa Baraza hilo kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara Mama ili kuleta ufanisi kiutendaji.
Uchaguzi wa Viongozi wa Baraza hilo ufanyika kila baada ya kipindi cha miaka miwili kwa kuwa na Wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar ambao kwa pamoja wanaunda wajumbe wa Baraza Kuu la Baraza hilo ambapo Mwenyekiti na Makamu wake wanaweza kutoka upande wowote wa Muungano, ikitokea mwenyekiti katokea Zanzibar inabidi Makamu wake pia atokee huko ili Katibu atoke Tanzania Bara.
Viongozi walioshinda kwa nafasi ya Mwenyekiti ni Johel Festo kutoka Mkoa wa Mwanza, Makamu Mwenyekiti ni Aidath Ismail pia kutoka Mkoa wa Mwanza, Katibu ni Thuwaiba Abdallah anayetokea Unguja Magharibi na viongozi hao utadumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku amemtaka Mwenyekiti mpya wa Baraza la Watoto Taifa kuhakisha anaongeza idadi ya mabaraza katika ngazi ya Mkoa na Wilaya na kumtaka kufanya hivyo kwa kushirikiana na Wizara ili kila mkoa upate uwakilishi wake.
Wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii muda mchache kabla ya kuanza uchaguzi wa viongozi wa Baraza hilo Kitaifa.
Mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Watoto akikusanya kura kutoka kwa wajumbe wa Baraza wakati wa zoezi la kuwapigia kura wagombea wa uongozi wa Baraza la Taifa la Watoto.
Baadhi ya Wagombea wa uongozi katika Baraza la Watoto Taifa wakisubiri matokeo kujua kama bahati iko upande wao wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Watoto jana katika Manispaa ya Singida.
Viongozi wa nafasai nne za juu za Baraza la Taifa la Watoto wakiwa tayari kwa majukumu mapya wakawanza kushoto ni mweka hazina mpya wa Baraza hilo Ince Frank kutoka mkoa wa Mbeya, wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Aidathi Ismail kutoka Mkoa wa Mwanza na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Joel Festo kutoka Mkoa wa Mwanza na kulia kwake ni Katibu wa Baraza Thuwaiba Abdallah kutoka Unguja Magharibi.
Hivyo makala WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO
yaani makala yote WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wajumbe-baraza-la-watoto-taifa-wachagua.html
0 Response to "WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO"
Post a Comment